• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 8:55 PM
Mwanamke ashtakiwa kutwaa bidhaa baada ya mwanamume aliyemburudisha kimapenzi kukosa kumlipa

Mwanamke ashtakiwa kutwaa bidhaa baada ya mwanamume aliyemburudisha kimapenzi kukosa kumlipa

Na JOSEPH NDUNDA

MWANAMKE ambaye alichukua televisheni, saa ya mkononi na simu, zote za thamani ya Sh59,100 kutoka kwa mwanaume ambaye alikosa kumlipa baada ya kummegea ‘tunda’ jana alishtakiwa kwa kosa la wizi kwenye Mahakama ya Makadara.

Mwanamke huyo, ambayo amepewa jina la EWM, 38 pia alishtakiwa kwa kutoa Sh3,880 kutoka kwa akaunti ya Mpesa ya mwanaume huyo, JKM. Aliiba televisheni, saa na simu katika eneo la Masimba, Kayole Nairobi usiku wa Oktoba 24/25.

Korti ilielezwa kuwa JKM alikuwa akijiburudisha kwa kileo klabuni, mwanamke huyo alipofika akamwalika waketi meza moja ili wanywe pamoja. Wawili hao kisha waliondoka na kuenda kwa nyumba ya EWM  lakini mwanamke akataka waongeze pombe ndipo tena wakaenda kwenye baa jingine na kununua pombe nyingi.

Waliporejea kwa nyumba na kuendelea kunywa, JKM aliomba azime kiu chake cha mapenzi lakini mwanamke huyo akasema lazima angelipwa Sh5,000 kwa huduma hiyo.

Anadai kuwa baada ya kugawiwa ‘vitu’ kishujaa, JKM alikataa kulipa na wawili hao wakalemewa na usingizi.

Mwanamke huyo aliwaeleza polisi kuwa JKM alimpa nambari yake ya siri ya Mpesa lakini akabaini alikuwa na pesa kidogo ambazo hazikufikisha Sh5,000 walizoelewana.

Baada ya kuamka saa moja asubuhi, mshukiwa alibeba televisheni na bidhaa nyingine kisha kuondoka. Aliwaambia polisi kuwa aliuza televisheni hiyo kwa mhudumu anayeuza vifaa vya kielektroniki.

Alikamatwa baada ya kuonekana kwenye baa moja ambapo walikuwa wakinywa na JKM.

Mbele ya Hakimu Mkuu  Tito Gesora, aliwaachiliwa kwa dhamana ya Sh40,000 au pesa taslimu Sh30,00 huku kesi hiyo ikitarajiwa itatajwa mnamo February 9 kabla ya kuanza kuskiziwa Juni 24 mwaka ujao.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi wenye maduka Toi Market, Kibera wamejipanga kwa mkasa...

Akothee aliyeoga na kurudi soko, ametwaliwa tena na...

T L