• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mwanamke mashakani kwa kuficha ‘dume’ mbakaji

Mwanamke mashakani kwa kuficha ‘dume’ mbakaji

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE aliyeficha habari kwamba msichana wa miaka 15 aliyetoroka kwa mama yake alikuwa akiishi na mwanaume aliyemfahamu ameshtakiwa.

Jane Wambui Njeri alishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Agnes Mwangi kwa kuficha habari muhimu kuhusu binti wa jirani yake.

Hakimu alifahamishwa kuwa Wambui alijua msichana huyo wa miaka 15 alikuwa akiishi na mvulana katika kitongoji cha Soweto eneo la Embakasi Mashariki, lakini alimficha mama ya binti huyo.

Wambui alishtakiwa kwa kusaidia mvulana kutekeleza kitendo cha ubakaji.

Iwapo Wambui atapatikana na hatia chini ya kifungu cha sheria nambari 396 (1) na 397 atafungwa miaka mitatu gerezani.

Sheria hizi zinakataza mmoja kusaidia kuficha uhalifu uliotendeka akijua walioutekeleza.

Wambui alikana kutekeleza uhalifu huo mnamo Mei 15, 2023

Inadaiwa Wambui alimtambulisha msichana huyo kwa mwanaume huyo kwa jina Irungu.

Mama ya msichana huyo alienda kwa Wambui kuuliza ikiwa alimwona lakini akakana ilhali huku alikuwa anajua aliko bintiye.

Msichana huyo aliokolewa na polisi kisha akafichua ukweli kwamba ni Wambui aliyemwelekeza kwa Irungu.

Wambui aliachiliwa kwa dhamana ya Sh45, 000.

Kesi itaanza kusikizwa Julai 7, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Washtakiwa kwa wizi wa samaki

Wanaharakati wa mazingira wapigwa jeki mradi wa Sh20...

T L