• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Mwaniaji urais apoteza kesi na kuomba chupa ya maji

Mwaniaji urais apoteza kesi na kuomba chupa ya maji

NA RICHARD MUNGUTI

MWANIAJI kiti cha urais ambaye kesi ya kupuinga kuidhinishwa kushiriki katika uchaguzi wa Agosti 9,2022 aliomba apewe chupa ya maji avunje kiu na pia asitoke kortini bila kitu.

Bw Stephen Owuoko alisababisha kicheko cha kishindo katika jopo la kuamua mizozo ya kuidhinishwa kwa wawaniaji viti katika uchaguzi mkuu ujao (DRC) alipoitisha maji.

Akasema Bw Owuoko: “Kwa vile kesi yangu ya kuomba uamuzi wa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) Wafula Chebukati kukataa kuniidhisha nishiriki kinyang’anyiro cha urais naomba nipewe chupa ya maji nisitoke mahakamani mkono tupu. Nitayakunywa nimeze hasira nya kupoteza mara mbili azma yangu ya urais”

Hakukomea hapo, Bw Owuoko aliwapongeza wanachama wa jopo hilo Wambua Kilonzo, Justus Nyangaya na Irene kwa kutoa uamuzi uliomridhisha.

“Nawapongeza kwa kutoa uamuzi ulioniridhisha ikitiliwa maanani mlikuwa na kesi 300 na zote mmeziamua. Hamkulala hata katika muda wa siku 10,” alisema Owuoko.

Pia alisababisha kicheko tena akisema: “Kama ningeshinda urais ningekufanya wewe (Wambua Kilonzo) mwanasheria mkuu kwa vile wewe uko na roho safi na uko na ukwasi wa sheria. Umenieleza nikaridhika sababu ya kung’atuliwa kinyang’anyironi cha mbio za kuenda Ikulu.”

Alisema kwa ujumla Kilonzo, Nyang’aya na Masitsi waliendeleza jopo hilo kwa uchagamfu na furaha.

“Naomba Mungu awabariki katika kazi zenu za kuhakikisha haki imetendeka,” Bw Owuoko aliomba.

“Amen (Amina),” Bw Kilonzo alijibu.

Bw Chebukati alikataa kuidhinisha Bw Owuoko kuwania urais kwa vile hakuwasilisha karatasi zake katika muda uliofaa.

Pia hakuwa na karatasi alipofika mbele ya Chebukati akisema mnamo Mei 29, 2022 alizuiliwa na maafisa wa ulinzi katika lango la Ukumbi wa Bomas.

Aliacha stakabadhi zake katika afisi ya IEBC Bomas lakini hakusema alimwachia nani.

Hakuweza kupata sahihi za wapiga kura 48,000 kutoka kaunti 24 kuunga mkono azma yake ya urais.

Jopo hilo lilikubaliana na Chebukati kuwa Owuoko hajahitimu.

Punde tu baada ya kusoma uamuzi wao, Owuoko aliomba maji.

Kesi nyingine ya mwaniaji mwingine wa kiti cha urais James Kamau mwenye umri wa miaka 31 iliisha kwa yeye kuambulia patupu.

Hakutimiza masharti ya kuwania urais.

  • Tags

You can share this post!

Wanasiasa wajiuza kwa jina la Mungu

Novartis yawekeza Sh30 bilioni kukomesha malaria na...

T L