• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 7:52 PM
NTSA yatayarisha sheria ya kudhibiti sekta ya bodaboda

NTSA yatayarisha sheria ya kudhibiti sekta ya bodaboda

NA MANASE OTSIALO

MAMLAKA ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) iko mbioni kutayarisha sheria ya kudhibiti sekta ya uchukuzi wa bodaboda.

Akizungumza akiwa Garissa, mwenyekiti wa NTSA, Bw Aden Noor alifichua kwanba shirika hilo linaandaa sheria ya kulazimisha kila mhudumu wa bodaboda kuwa mwanachama wa chama cha akiba na mikopo (SACCO) kilichosajiliwa kama ilivyo kwa sekta ya matatu.

“Tunataka bodaboda wote wawe katika vyama vya akiba na mikopo ili tuweze kufahamu ni nani anafanya nini na wapi,” alisema.

Bw Noor alisema NTSA itaanza kutumia huduma za kibinafsi za kukagua magari iwapo sheria mpya itapitishwa.
Sheria hiyo inapendekeza sekta ya kibinafsi iruhusiwe kuanzisha kampuni za kukagua na kupendekeza magari ya kutumiwa barabarani.

Kulingana na Bw Noor, kuwa na mashirika mengi yanayotoa huduma za kukagua magari kutapunguza ajali za barabarani.

Alisema pia hatua hiyo itapunguza msongamano katika vituo vya NTSA na muda unaotumiwa na wamiliki wa magari wakati wa ukaguzi.

“Hii itasaidia kupunguza ajali kwa kuhakikisha kila gari liko katika hali nzuri ya kuwa barabarani kote nchini,” alisema.

Bw Ali alisema ni vigumu kujua hali ya gari bila kuwa na cheti cha ukaguzi.

“Ninaomba Wakenya wote kuzingatia sheria za trafiki wakiwa barabarani na pia wapeleke magari yao kukaguliwa kabla ya kuyaingiza barabarani. Hii itaokoa maisha ya watu wengi,” alisema.

Iwapo mswada huo utapitishwa kuwa sheria, basi sekta ya kibinafsi itaweza kuanzisha kampuni za kukagua na kupendekeza magari kutumika barabarani.

Mswada wa NTSA 2022 ambao kwa sasa uko katika awamu ya kushirikishwa kwa umma, utaruhusu shirika hilo kutafuta huduma za kukagua magari kutoka sekta ya kibinafsi tofauti na sasa ambapo ndilo linakagua magari.

Itakuwa ni makossa kuendesha au kumiliki gari bila cheti cha ukaguzi. Vile vile, itakuwa ni makossa kubadilisha cheti cha ukaguzi kinachotolewa na NTSA au shirika lilingine lolote linaloidhinishwa kufanya ukaguzi wa magari na kutoa cheti.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali ianze upesi ujenzi wa mabwawa 200...

Ruto akaribia kumpokonya Uhuru chama cha Jubilee

T L