• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Nyumba 80 zateketea Mukuru, wakazi 200 wakilazimika kuvumilia mvua, baridi kali

Nyumba 80 zateketea Mukuru, wakazi 200 wakilazimika kuvumilia mvua, baridi kali

NA SAMMY KIMATU

WATU zaidi ya 200 walivumia baridi kali usiku baada ya nyumba 80 kuteketea usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Naibu kamishna kaunti ndogo ya Starehe Bw John Kisang amesema moto mkubwa ulitokea katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Hazina, South B mwendo wa saa nane za usiku.

Mwathiriwa, Bw Nicholas Koyo,48, aliyekuwa na biashara ya kushona nguo amesema amepoteza mali ya zaidi ya Sh500,000 kwenye mkasa huo.

Moto huo ulitokea dakika chache tu baada ya stima kurudi.

Mnamo Alhamisi jioni, mvua kubwa ilinyesha ikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi huku nyumba kadhaa zikianguka, likiwemo darasa moja la shule ya Msingi ya St Catherine.

Kando na hayo, mabati yaliyojenga ua wa ofisi ya msaidizi wa kamishna South B yaling’olewa na upepo.

Katika Kituo cha Watoto wenye Ulemavu cha Songa Mbele, mti mkubwa ulianguka ndani ya kituo ila kwa bahati nzuri watoto walikuwa wamepelekwa nyumbani.

Mtaani Kayaba, nyumba mbili ziling’olewa mapaa yake sawia na nyumba nyingine nne katika mtaa wa Mariakani.

  • Tags

You can share this post!

Mjadala mkali Mama wa Taifa akimualika nchini mwinjilisti...

Rais wa Ghana aambia Wazungu walipe Afrika kwa utumwa wa...

T L