• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 3:31 PM
Ogoti azimwa kusikiza kesi dhidi ya gavana Njuki na mkewe

Ogoti azimwa kusikiza kesi dhidi ya gavana Njuki na mkewe

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA kuu imemzima hakimu mkuu Douglas Ogoti kusikiza na kuamua kesi ya ufisadi wa Sh34milioni inayomkabili Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki na mkewe Margaret Mugweru.

Mbali na wawili hao (njuki na Margaret) kuna maafisa tisa wa serikali ya kaunti ya Tharaka Nithi na washtakiwa wengine kutoka familia moja. Washtakiwa wengine walioshtakiwa kutoka familia moja ni Kenneth Mucuiya na mkewe Caroline Wambui pamoja na Bw Japheth Gitonga ambaye ni ajenti wao wa masuala ya  Benki na pia msaidizi wao kazini.

Jaji James Wakiaga alimwamuru Bw Ogoti asisikize kesi hiyo alipoamuru kesi hiyo ya ufisadi ihamishwe kutoka mahakama ya kuamua kesi za ufisadi ya Milimani Nairobi hadi korti ya Embu.

Akiamuru Bw Ogoti akome kuendelea na kesi hiyo, Jaji Wakiaga, alisema hakimu huyo aliyehamishwa kutoka Nairobi hadi mahakama ya Embu alikuwa akiishughulikia akiwa jijini Nairobi.

Bw Njuki ameshtakiwa na watu wengine 20. Jaji Wakiaga anayesimamia kitengo cha mahakama kuu cha kushughulikia kesi za ufisadi alisema Bw Njuki na wenzake wangelishtakiwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya Embu.

  • Tags

You can share this post!

Mjakazi akana kuiba mkufu na pesa za mwajiri wake

KAMAU: Uchawi: Tamaduni za jadi zinadunisha jamii

T L