• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Mjakazi akana kuiba mkufu na pesa za mwajiri wake

Mjakazi akana kuiba mkufu na pesa za mwajiri wake

Na RICHARD MUNGUTI

MJAKAZI aliyetoroka kutoka kwa mwajiri wake ameshtakiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh140,000 na mkufu wa thamani ya Sh3000.

Alipofikishwa mbele ya hakimu mkazi  Charles Mwaniki, Irene Andanu, alidai aliteswa na kudhulumiwa na maafisa wa polisi waliomtia  nguvuni. Irene alieleza Bw Mwaniki kuwa polisi walimfungia ndani ya nyumba ya mwajiri wake Bi Joy Mbeche kwa siku nzima kabla ya kupelekwa kituo cha polisi.

Irene alikabiliwa na shtaka la kuchomoka na pesa hizo za mwajiri wake alipomaliza kuosha chumba cha kulala na kupanguza kabati yake vumbi. Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa aliiba pesa hizo Oktoba 7,2021 katika mtaa  wa Mountain View kaunti ndogo ya Westlands, Nairobi.

Polisi walisema mshtakiwa alipata pesa hizo na mkufu huo kutokana na kazi yake. Mahakama ilifahamishwa mshtakiwa aliyeajiriwa Septemba 15, 2021 kuwa anafanya kazi siku nne kwa wiki kati ya saa mbili asubuhi na saa 12 jioni.

Mlalamishi alikuwa jikoni akiendeleza mapishi mshtakiwa alipokuwa akifanya kazi katika chumba chake cha kulala. Baada ya kuchana mbuga na pesa hizo mshtakiwa alitoweka hadi alipokamatwa Oktoba 14, 2021.

Bi Mbeche aligudua pesa, mkufu wake na pete ya harusi hazimo alipokua akitaka kuivaa. Mjakazi huyo alikanusha shtaka na  kuachiliwa kwa dhamana ya Sh200,000 pesa tasilimu hadi Novemba 1,2021 kesi itakaposikizwa.

 

  • Tags

You can share this post!

Awara amlewesha Mganda na kumpora Sh130,000

Ogoti azimwa kusikiza kesi dhidi ya gavana Njuki na mkewe

T L