• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Papa ateua Muheria Kaimu Askofu wa Embu

Papa ateua Muheria Kaimu Askofu wa Embu

NA PIUS MAUNDU

KIONGOZI wa Kanisa la Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, amemteua Askofu Mkuu Anthony Muheria wa Nyeri kuongoza Dayosisi ya Embu hadi askofu wa kudumu atakapoteuliwa.

Haya yamejiri baada ya Askofu Paul Kariuki kuteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa dayosisi mpya iliyobuniwa ya Makueni.

Bw Kariuki alikuwa Askofu wa Dayosisi ya Embu kwa miaka 14, hadi Julai alipoteuliwa na Papa Francis kusimamia Dayosisi ya Makueni ambayo ni mpya kabisa.

“Tayari tumeanza mchakato wa kutafuta askofu mpya wa Dayosisi ya Embu, hivyo basi askofu yeyote anayehisi mwito wa kuwa askofu anaweza kutuma maombi.”

“Kwa sasa, kwa vile kuna pengo, Baba Mtakatifu ameteua Askofu Mkuu Anthony Muheria, aliyewahi kuhudumu kama askofu wa Embu miaka kadhaa iliyopita,” alisema Mwakilishi wa Papa Francis nchini Kenya na Sudan Kusini, Hubertus Maria Van Megen akiwa mjini Wote, Kaunti ya Makueni, mnamo Jumamosi, Septemba 30, 2023.

“Tunatumai chini ya uongozi wake, Dayosisi ya Embu itaendelea kukuza mbegu ambazo Askofu Kariuki tayari amepanda.”

 

  • Tags

You can share this post!

Majengo ya mamilioni ya pesa Eldoret kubomolewa kuigeuza...

Kampuni yamlilia Gachagua kuisaidia kurejeshewa ardhi...

T L