• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 10:18 AM
Penzi la mubaba tamu nashindwa kumuacha

Penzi la mubaba tamu nashindwa kumuacha

SHANGAZI;

Mpenzi wangu ni mume wa mtu. Ana umri wa miaka 46 nami nina miaka 28. Penzi lake tamu limenizuzua na sijui kama naweza kupenda mwanamume mwingine, ingawa nataka kuolewa.

Kama kweli una matumaini ya kuolewa ni lazima ubadili msimamo wako kuhusu uhusiano huo. Ukubali huyo ni mume wa mtu na hawezi kuwa wako. Pili, unaweza kupata mwingine mwenye penzi tamu hata zaidi. Uamuzi ni wako.

Ex ameganda kwangu hajali kuwa mke wa 2

Mwanamke aliyekuwa mpenzi wangu hajassita kunipigia simu akisema ameshindwa kupenda mwingine. Anajua nimeoa lakini anaomba tuwe wapenzi akiahidi kuweka siri uhusiano wetu. Waonaje?

Uhusiano ambao mwanamke huyo anataka unakiuka madili ya ndoa. Labda amegundua bado una hisia kwake ndiposa ameshindwa kukusahau. Kama hutaki kumsaliti mkeo mwambie wazi huwezi ili atoe mawazo yake kwako.

Tangu nimjulishe kwa rafiki amebadilika

Juzi nilijulisha mpenzi wangu kwa demu rafiki yangu. Waliongea sana na kubadilishana namba za simu. Tangu siku hiyo amekuwa baridi kwangu.

Mabadiliko hayo yanahusu huyo rafiki yako. Inaonekana alimvutia zaidi na ameamua kukuacha kwa mataa kwa ajili yake. Kama ni hivyo itabidi ukubali tu. Lakini pia zungumza na mpenzi wako ili uthibitishe.

Ndoa ilikuwa njiani sasa nimeingia wasiwasi

Nilikuwa na matumaini makubwa kwamba nitamuoa mpenzi wangu. Hata hivyo, nimeanza kukata tamaa sababu ya mienendo yake. Siku za hivi majuzi ameanza kuniepuka. Sielewi kwanini na sijamkosea.

Ni mpenzi wako tu anayeweza kuweka wazi msimamo wake kuhusu uhusiano wenu. Kama hujamuuliza muhimu ufanye hivyo. Inawezekana ameamua kujiondoa lakini anashindwa kusema.

>>Usikose safu hii kila Jumatatu hadi Ijumaa saa nne usiku -Mhariri

  • Tags

You can share this post!

El-Nino: Wakazi sasa watakiwa kuhamia maeneo salama

Karen Nyamu: Ruto ndiye ameumia zaidi na kupanda kwa bei ya...

T L