• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Pigo kwa wahubiri YouTube ikitangaza kufutilia mbali video za ‘maombi ya uponyaji kansa’

Pigo kwa wahubiri YouTube ikitangaza kufutilia mbali video za ‘maombi ya uponyaji kansa’

Na WANGU KANURI

HUENDA ukawa umepatana na video za maombi ya uponyaji katika mtandao wa kijamii haswa YouTube unapopekua.

Video hizi huonyesha mgonjwa wa kansa, ukimwi au hata mtu mwenye ulemavu akiponywa baada ya kuamini.

Huku video hizi zikinuiwa kutia watu nguvu na moyo wanapokuwa kwenye hali hii ngumu ya kiafya, wengi wamekataa kuzuru hospitali kutibiwa kwa kuamini ‘wataponywa.’

Ni kwa sababu ya upotoshaji huu ambao YouTube imeahidi kutoa video zote za uponyaji haswa ya magonjwa ya kansa mtandaoni katika wiki zijazo.

Mtandao huo wa kijamii ulisema kuwa, “Kwa siku na wiki zijazo, tutaondoa video zote zinazoeleza kuhusu matibabu ya kansa ambazo si za kweli na zinapotosha wagonjwa kwa kuwafanya wasitafute matibabu.”

Video hizo pia ni pamoja na zile zinazowashauri wagonjwa hao wa kansa kutumia kitunguu saumu au kula vyakula vyenye vitamini C badala ya kupata matibabu kwa njia ya mtambo wa kisasa unaotoa miale ya X-Ray kuua seli zinazosambaza saratani (radiotherapy).

“Pia tutaweka kizuizi cha umri au kuwa na paneli ya watu watakaoangazia maudhui ya video ili kuongezea ujumbe uliopo,” YouTube ikasema.

  • Tags

You can share this post!

Agizo baa karibu na shule, makazi zifungwe

Wahudumu wa zamani wa NMS walia kuachwa kwa mataa

T L