• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Wahudumu wa zamani wa NMS walia kuachwa kwa mataa

Wahudumu wa zamani wa NMS walia kuachwa kwa mataa

NA WINNIE ONYANDO

WAHUDUMU wa afya wa Kaunti ya Nairobi ambao walihudumu chini Idara ya Huduma za Jiji (NMS) iliyovunjiliwa mbali, sasa wanalia wakisema wameachwa kwa mataa.

Kwenye Barua ya Wazi iliyochapishwa na wafanyakazi hao katika gazeti la Daily Nation Ijumaa Agosti 18, 2023, wafanyakazi hao wanaomba serikali ya Rais William Ruto na ya Gavana Johnson Sakaja kushughulikia maslahi yao.

Wahudumu hao 1,350 kutoka kwa idara mbalimbali ya Wizara ya Afya ya Kaunti ya Nairobi wanasema serikali ya Sakaja imewatelekeza.

“Tunamwomba gavana kutimiza ahadi yake ya kuwaajiri wafanyakazi wa NMS. Pia tunapinga unyanyasaji,” kundi hilo likasema.

Mnamo Januari 2023, Gavana Sakaja aliagiza wafanyakazi wa zamani wa NMS ambao kandarasi zao ziliisha kutuma maombi yao ya kazi na hata kuahidi kuwaajiri.

“Niliagiza kwamba maafisa wote wa zamani wa NMS ambao kandarasi zao na NMS ziliisha kuripoti kazini mara moja na kulipwa ada zao ambazo hazijakamilika. Tutawapa kipaumbele hasa katika ajira,” gavana huyo alisema.

Hata hivyo, ni wazi kuwa hilo halijatendeka.

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa wahubiri YouTube ikitangaza kufutilia mbali video...

Uzee sio uchawi, lasema shirika likikemea mauaji ya...

T L