• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:44 PM
Polisi wachunguza kisa cha mwalimu kuita mwanafunzi atumbuize wageni kumbe anamnyemelea

Polisi wachunguza kisa cha mwalimu kuita mwanafunzi atumbuize wageni kumbe anamnyemelea

NA RUTH MBULA

POLISI Kisii wanachunguza kisa kimoja ambapo inadaiwa mwalimu mmoja wa kiume alimuitwa mwanafunzi kuenda kutumbuiza wageni nyumbani kumbe anamnyemelea.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alisema Jumamosi kwamba amepata ripoti ya suala hilo.

Wazazi wa msichana huyo wa shule ya msingi ya  St Dominic Chisaro iliyoko eneobunge la Bonchari wamelaumu polisi wakidai kwamba walimzuilia msichana huyo kwa seli ya kituo cha polisi cha Suneka baada ya kunajisiwa na mwalimu husika.

Inadaiwa mwanafunzi huyo alikuwa amefukuzwa shuleni kwa sababu wazazi wake hawakuwa wamelipa pesa za chakula cha mchana.

Lakini Kamanda wa Polisi Kisii Bw Charles Kases aliambia Taifa Jumapili kwamba msichana huyo alikuwa hospitalini mnamo Alhamisi akitibiwa na hawangemuacha kurejea nyumbani usiku kwa sababu za kiusalama.

“Tuna fomu yake ya P3 na anaruhusiwa kuenda nyumbani kwa wazazi wake leo (jana Jumamosi) na mshukiwa atapelekwa kortini mnamo Jumatatu,” akasema Bw Kases akipuuzilia mbali madai ya wazazi wa mdhulumiwa.

Wazazi wa mwanafunzi huyo walidai alifukuzwa shuleni kuenda kuleta pesa za chakula cha mchana lakini mwalimu ‘akamteka’ aende amsaidie kutumbuiza wageni wake ndipo kisa hicho cha unajisi kikafanyika.

  • Tags

You can share this post!

Wanahabari wa NMG wazoa tuzo za OFAB-Kenya

Mwangaza ajipata gizani Kindiki akipiga stopu vikao maarufu...

T L