• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Polisi wazuia raia kuchota mafuta lori lingine likianguka

Polisi wazuia raia kuchota mafuta lori lingine likianguka

Na RUSHDIE OUDIA

POLISI Kaunti ya Kisumu waliweka ulinzi mkali kuzuia wananchi kukaribia lori lililoanguka likiwa limebeba mafuta katika daraja la Kasagam.

Kisa hicho kinajiri siku mbili baada ya wakazi 15 kufariki, moto ulipowaka wakichota mafuta kwenye lori lililoanguka Kaunti ya Siaya.Polisi walisema walichukua hatua za haraka kulinda lori hilo, lililoanguka mwendo wa saa moja na nusu jioni.

Ajali hiyo ilitokea wakati dereva alikuwa akikata kona kali katika barabara kuu ya Kisumu-Nairobi.Kamanda wa polisi kaunti ya Kisumu Samuel Anampiu aliongoza maafisa kufunga eneo la ajali ili wakazi wasikaribie lori kuchota mafuta ilipofanyika kwenye ajali iliyotokea Malanga kaunti ya Siaya Jumatatu.

Polisi walisema kwamba dereva wa lori alitoroka baada ya ajali.“Dereva wa lori hapatikani na juhudi za kumtafuta zinaendelea,” alisema Bw Anampiu. Wazima moto walifika katika eneo la mkasa wakiandamana na maafisa wa shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi na Usalama na wa Mamlaka ya Kuthibiti Kawi na Mafuta.

Kufikia jana, mafuta yalikuwa yakimiminika kutoka lori hilo na kuingia katika mto unaoelekeza maji Ziwa Victoria.“Tunasikitika kwamba viumbe wa majini wanahatarishwa na tutashirikiana na Mamlaka ya Taifa ya Kulinda Mazingira kukadiria kiwango cha uchafuzi na hatua za kuzuia tunazoweza kuchukua kuhakikisha hatari imepunguzwa,” alisema Bw Anampiu.

  • Tags

You can share this post!

Watu 8 wauawa katika mashambulizi baada ya ziara ya...

Kiongozi wa upinzani TZ azuiliwa usiku wa manane