• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
Pombe haramu sasa yauzwa vyooni kukwepa polisi

Pombe haramu sasa yauzwa vyooni kukwepa polisi

ERIC MATARA Na STEVE NJUGUNA

WAUZAJI pombe haramu katika kaunti za Nakuru, Nyeri, Nyandarua na Laikipia wamebuni mbinu chafu ya kuendesha biashara hiyo ili wakwepe operesheni ya kuimaliza iliyoamrishwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Uchunguzi huru ulioendeshwa na Taifa Leo sasa umebaini waendeshaji wa biashara hiyo haramu sasa wanauza pombe hizo ndani ya vyoo, misituni, kwenye mabonde, vichochoroni na sehemu nyingine fiche ili kukwepa mtego wa polisi.

Wauzaji wa pombe haramu katika maeneo kama vile Molo, Njoro, Bahati, Kuresoi Kusini, Kuresoi Kaskazini na mitaa kadhaa ya mji wa Nakuru wanaendesha biashara hiyo katika sehemu za kiajabu kama vile makaburini na ndani ya vyoo.

Mjini Nakuru, biashara hiyo sasa inanawiri katika makaburi ya Nakuru Kusini na Nakuru Kaskazini.

“Wafanyabiashara hao hupakia pombe hizo kwenye sacheti na mikebe na kuziuza hadharani maeneo ya makaburi badala ya kuziuza katika vyumba ambavyo maafisa wa polisi na utawala wamezoea,” akafichua John Kimani, mfanyabiashara jijini Nakuru.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yatangaza nia ya kukata wafanyakazi asilimia 3 ya...

Kaunti 5 kushirikiana kuzima wizi wa dawa

T L