• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:15 PM
Raia wa Cameroon asukumwa gerezani kwa ulaghai wa dhahabu

Raia wa Cameroon asukumwa gerezani kwa ulaghai wa dhahabu

Na RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Cameroon aliyemlaghai raia wa Iran Sh53.8 milioni ameshtakiwa katika Mahakama ya Milimani.

Annouar Mohammed Sadate aliyeshtakiwa mbele ya hakimu mkuu Lucas Onyina alikana kumlaghai Ismail Kolawole Adesina Sh53, 828, 400 akijifanya kampuni yake ya Miles Outlets Limited (MOL).

Alidai kuwa kampuni hiyo ingemsafirishia kwa ndege kilo 33 za dhahabu kutoka Kenya hadi Dubai.

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda alipinga Annoar akiachiliwa kwa dhamana kwa vile “alitiwa nguvuni katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mnamo Mei 7, 2023 akijaribu kutoroka.”

Bw Onyina aliamuru mshtakiwa azuiliwe katika gereza la Viwandani hadi Mei 17, 2023 kesi itakapotajwa tena.

Gikunda alisema kesi dhidi ya Annouar itaunganishwa na nyingine.

  • Tags

You can share this post!

Masaibu: Pasta Ezekiel ‘afungiwa’ akaunti zake...

Yesu wa Tongaren mashakani akiagizwa kufika kwa polisi

T L