• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Yesu wa Tongaren mashakani akiagizwa kufika kwa polisi

Yesu wa Tongaren mashakani akiagizwa kufika kwa polisi

Na JESSE CHANGE

KIONGOZI wa Kanisa la New Jerusalem Eliud Wekesa, maarufu kama “Yesu wa Tongaren” ameamriwa kufika kwa polisi Bungoma ahojiwe kuhusiana na mafunzo ya kanisa lake.

Kamanda wa Polisi wa Bungoma Francis Kooli Jumatatu, Mei 8, 2023, alimtaka Wekesa kujiwasilisha katika kituo cha polisi cha Bungoma Jumatatu “baada ya malalamishi kuibuliwa kwamba anatoa mafunzo ya itikadi kali kama Mhubiri Paul Mackenzie wa Kilifi”.

“Yesu wa Tongaren” amejipata mashakani wiki moja baada ya Gavana wa Bungoma Ken Lusaka kushauri Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imchunguze kuhusiana na tuhuma za kutoa mafunzo yenye itikadi kali kwa waumini wa Kanisa lake.

Akiongea na wanahabari nyumbani kwake eneo la Kamukunya, Bw Lusaka alimkashifu vikali Bw Wekesa kwa kujiita “Yesu” akisema anafaa kuchunguzwa kubaini “ikiwa anatoa mafunzo ya kiitikadi kama Pasta Paul Mackenzie anayehusishwa na mauaji ya halaiki Shakahola.”

Haya hivyo, Jumatatu, Bw Wekesa aliwasihi polisi wasimkate akisema hana hatia yoyote.

Wiki jana, Rais William Ruto aliunda jopo kazi la kuchunguza kanuni zinazoongoza usajili wa makanisa nchini ili kubaini yale ambayo yalianzishwa kinyume cha sheria.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

Raia wa Cameroon asukumwa gerezani kwa ulaghai wa dhahabu

Viongozi sasa waomba Gavana Natembeya ‘atembee...

T L