• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Raia wa Rwanda na Mkenya wafika kortini kung’ang’ania Sh400 milioni

Raia wa Rwanda na Mkenya wafika kortini kung’ang’ania Sh400 milioni

NA RICHARD MUNGUTI

RAIA wa Rwanda na Mkenya wanang’ang’ania Sh400 milioni zilizotokana na biashara ya kuuza bidhaa katika mitandao.

Mahakama ya Milimani iliamuru Jumatatu kwamba akaunti za kampuni ya Stay Online Limited zifungwe hadi pale Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai (DCI) itabaini uhalisi wa pesa hizo.

Hakimu mwandamizi Bw Bernard Ochoi aliwaruhusu maafisa wa DCI muda wa siku 10 kukamilisha uchunguzi wao.

Bw Ochoi alitoa agizo baada ya kufahamishwa na kiongozi wa mashtaka James Gachoka kwamba polisi wamepokea ripoti kutoka kwa benki tatu Equity Bank Limited (EBL) na United Bank of Africa (UBA).

Katika ushahidi uliowasilishwa na mawakili Aranga Omaiyo, Danstan Omari na Cliff Ombeta, ilibainika kwamba pesa kiasi kikubwa zimekwama katika akaunti tatu zilizofunguliwa nchini Kenya kwa idhini ya mwekezaji wa kimataifa Desire Muhinyuza.

“Muhinyuza alianza kumshuku Koome Kirimi baada ya kuitisha kwa vitisho dola za Marekani 120,000   zitumwe katika akaunti yake iliyoko mjini Meru,” Bw Omari alieleza mahakama.

Kampuni ya Stay Online Limited (SOL) iko na matawi Rwanda, Uganda, Zambia na Canada.

Kirimi ndiye mwakilishi wa kampuni hiyo nchini Kenya.

  • Tags

You can share this post!

Cherargei ashambulia kamati ya NADCO kwa kukataa kusikiliza...

Walimu wataka Kilifi iorodheshwe kuwa mazingira magumu ya...

T L