• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Seneta wa zamani awasilisha kesi uchaguzi mkuu 2022 uhahirishwe hadi Novemba 28 2023

Seneta wa zamani awasilisha kesi uchaguzi mkuu 2022 uhahirishwe hadi Novemba 28 2023

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Seneta maalum Bw Paul Njoroge Ben amewasilisha kesi katika mahakama kuu akiomba uchaguzi mkuu wa 2022 uhahirishwe hadi Novemba 28 2023.

Katika kesi ya dharura aliyowasilisha Jumatatu katika mahakama kuu ya Milimani Bw Njoroge amesema tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) haikuwa na makamishna saba kama inavyotakiwa kisheria ilipotangaza uchaguzi mkuu ufanywe Agosti 9,2022.

Bw Njoroge anasema kuwa afisa mkuu mtendaji (CEO) IEBC ilipotangaza tarehe hiyo mpya ya uchaguzi pamoja na bajeti itakayotumika.

“Tarehe ya uchaguzi mkuu wa Urais, Ugavana , Useneta, Ubunge na Udiwani iliyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC ya Agosti 9, 2022 imelazimishiwa watu wa Kenya na IEBC na hivyo basi zoezi hilo ni haramu,” Bw Njoroge amesema.

Seneta huyo aliyekuwa anawakilisha watu walio na ulemavu katika bunge la Seneti kati ya 2013 na 2017 amesema kipindi cha Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake Dkt William Ruto chapasa kukamilika Novemba 28,2023 kwa kuwa waliapishwa kutwaa hatamu za uongozi Novemba 2017.

Katika ushahidi aliowasilisha mahakamani, Bw Njoroge alisema tayari IEBC ilianza harakati za kutangaza tenda ya kuchapisha kura, ununuzi wa vifaa vya dijitali zitakazotumika na kutangaza viwango vya pesa wanasiasa wanazopasa kutumia katika kampeini zao mwaka ujao.

Amesema IEBC imekiuka Katiba na sheria ilipotangaza bajeti ya kufadhili uchaguzi huo mkuu wa 2022 kama haina makamishna wote saba.Makamishna wanne walioteuliwa kuhitimisha idadi wawe saba ni Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Cherop, and Justus Abony.

Watatu walikuwa wanaendeleza shughuli za IEBC ni Wafula Chebukati (mwenyekiti), Boya Molu na Prof Abdi Yakub GuliyeBw Njoroge alisema tayari serikali imetenga mabilioni ya pesa ya walipa ushuru yatakayotumika kufadhili uchaguzi huo mkuu.

“Itakuwa ni ukiukaji wa sheria IEBC ikiendeleza uchaguzi huu ilhali haizingatii sheria iliyopo,” Bw Njoroge amesema.Katika kesi hiyo Bw Njoroge ameishtaki IEBC, Mwanasheria mkuu kwa niaba ya mawaziri wote 67, Waziri wa Hazina Ukur Yatani.

Katika kesi hiyo pia amewataja Rais Kenyatta, Dkt Ruto, Mkurugenzi wa Bajeti, Bunge la Kitaifa, Bunge la Seneti na Magavana.

 

  • Tags

You can share this post!

Wakewenza wakazia buda asali

Wandani wa Ruto wamjibu Tuju