• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 1:01 PM
Serikali kuanza kutoa chanjo ya ukambi kesho

Serikali kuanza kutoa chanjo ya ukambi kesho

Na MHARIRI

SERIKALI itaanza kesho kutoa chanjo ya ugonjwa wa ukambi-rubella (Measles-Rubella) katika kampeni inayolenga watoto milioni 3.5 katika kaunti 22.

Kampeni hiyo inayolenga watoto wa kati ya miezi tisa na miezi 59, itakamilika Julai 7, mwaka huu.Chanjo hiyo itatolewa bila malipo katika vituo 5,061 vitavyoweka maeneo ya umma kama vile sokoni, shuleni, maeneo ya ibada.

Wahudumu wengine wa afya watakuwa wakizunguka kwa lengo la kufikia idadi kubwa ya watoto.Kulingana na wizara ya Afya, visa vya maradhi ya ukambi-rubella vimeongezeka nchini katika miaka ya hivi karibuni.

Kaunti zinazolengwa katika kampeni hiyo ni Mandera, Wajir, Garissa, Baringo, Pokot Magharibi, Turkana, Kilifi, Tana River, Trans Nzoia, Elgeyo Marakwet, Busia, Homa Bay, Migori, Kisii, Kajiado, Nairobi, Bomet, Bungoma, Kakamega, Narok na Vihiga.

Uchunguzi uliofanywa nchini na serikali kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) ulibaini kuwa ukambi umekolea katika kaunti hizo 22. KNANaibu Waziri wa Afya, Mercy Mwangangi aliyekuwa akizungumza jijini Nairobi, aliwataka wazazi kupeleka watoto wao katika vituo hivyo ili wapewe chanjo hiyo bila malipo.

“Ukambi ni ugonjwa wa tatu unaoambukizwa katika kusababisha vifo vingi vya watoto. Vifo hivyo vinatokana na kuhara, homa ya mapafu, maambukizi ya masikioni (Otitis – media). Aidha, unaharibu ubongo na kusababisha upofu,” akaelezea.

Dkt Mwangangi alisema kuwa Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayokabiliwa na tishio kubwa la ugonjwa wa surua.Miongoni mwa kaunti ambazo zimeshuhudia mlipuko wa surua hivi karibuni ni Mandera, Wajir, Garissa, Pokot Magharibi na Tana River.

  • Tags

You can share this post!

Handisheki ni matunda ya uongozi mbaya – Mutua

Shule zakataa amri ya KNEC kuhusu mtihani