• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Shule zakataa amri ya KNEC kuhusu mtihani

Shule zakataa amri ya KNEC kuhusu mtihani

SHULE za umma na za kibinafsi zimelalamika dhidi ya sheria mpya kutoka kwa Baraza la Kitaifa la Mitihani (Knec) inayoamrisha shule zenye watahiniwa 40 kwenda chini kuwasajili katika shule jirani.

Walimu wakuu katika shule za umma na wamiliki wa shule za kibinafsi wanaitaka Wizara ya Elimu kuagiza Knec kubatilisha uamuzi huo kabla ya usajili wa mitihani kukamilika Julai 31. Usajili wa mitihani ya kitaifa kwa watahiniwa wa Darasa la Nane na Kidato cha Nne ulianza Juni 2.

Wamiliki wa shule za umma na kibinafsi jana walisema sheria hiyo inasababisha hali ya kuchanganyikiwa kwa sababu maelfu ya shule yana watahiniwa wanaopungua 40 waliopangiwa kufanya mitihani ya Cheti cha Shule ya Msingi (KCPE) na Cheti cha Shule ya Sekondari (KCSE).

Muungano wa walimu wakuu wa shule za msingi nchini (Kepsha) Johnson Nzioka jana alisema sheria hiyo inawahangaisha mno walimu wakuu hasa kutoka Maeneo yenye Ukame (ASAL) na mamia ya shule za vijijini. “Walimu wakuu wanashindwa kuelewa ni vipi watoto wataweza kusafiri masafa marefu kwenda kufanya mitihani katika shule nyinginezo,” alisema Bw Nzioka.

Alisema shule katika maeneo hayo zimetawanyika pakubwa huku nyingine zikiwa katika maeneo hatari hivyo basi kuunganisha vituo hivyo huenda kukahatarisha wanafunzi na walimu.Bw Nzioka alisema walimu wakuu pia wanashangaa ni kwa nini uamuzi muhimu kama huo ulifanywa bila kujadiliana na wasimamizi wa shule.

Alisema Kepsha imeanza kukusanya data ya shule zilizoathiriwa ili kuziwezesha kujadiliana na Wizara ya Elimu. Bw Nzioka alisema kwamba walimu wakuu pia wamechanganyikiwa kuhusu ni nani atakayekuwa msimamizi wa kituo ikiwa amri hiyo haitabadilishwa.Mkurugenzi wa Muungano wa Shule za Kibinafsi (Kepsa) Peter Ndoro alifichua kuwa amri hiyo inaathiri shule 3,800 za msingi na sekondari na watahiniwa 122,000.

“Tumemwandikia barua ya malalamishi Waziri wa Elimu, Prof George Magoha na Knec kwa kuwa agizo hilo lilitolewa bila majadiliano,” Ndoro. Mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu katika shule za watoto walemavu, Bw Peter Sitienei alisema karibu shule zote za SNE zina watahiniwa wasiofika 40.huku akiisihi Wizara kuzingatia kubatilisha agizo hilo.

  • Tags

You can share this post!

Serikali kuanza kutoa chanjo ya ukambi kesho

Ubaguzi: Weusi wafaa wajilaumu wenyewe