• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Serikali kutambua rasmi vazi la uponyaji la Mijikenda lililokuwa hatarini kuibwa

Serikali kutambua rasmi vazi la uponyaji la Mijikenda lililokuwa hatarini kuibwa

NA MAUREEN ONGALA

WAZIRI wa Jinsia Aisha Jumwa amesema serikali ya kitaifa imelinda rasmi vazi la jamii ya Mijikenda la Kishutu.

Vazi hilo la kishutu lilikuwa katika hatari ya kuibwa na jamii zingine, zikiwemo za kimataifa, kwa sababu ya kukosa kuandikishwa kama vazi linalotoka Pwani.

Akizungumza katika hafla ya kusherekea vazi hilo katika uwanja wa Karisa Maitha, Bi Jumwa alisema wakati umefika kwa Mijikenda kufaidika kiuchumi kutokana na Kishutu.

“Kishutu ni kitambulisho chetu kama jamii ya Mijikenda na muhimu kwa sababu tunawaenzi wale walioanza kutumia kwa uponyaji, shujaa Mekatlili wa Menza na nabii Mepopho,” akasema.

Kishutu ilitumika kwa uponyaji na inaaminika ya kuwa wanawake walipona maradhi ya mgongo na kiuno pindi walipojifunga kwa kiuno.

Vazi hilo lilitumika pia kwa kutoa mapepo.

Bi Jumwa alisema serikali ameweka mikakati ya kukabidhi serikali ya kaunti rasmi Kishutu na mali ingine ya Mijikenda baada ya kuorodheshwa na shirika la Makavazi nchini.

Afisa Mkuu wa wakfu wa Kishutu Bi Epi Chari alisifu hatua ya serikali ya kitaifa kutambua kishutu ni mwamko mpya kwa jamii ya Mijikenda na kusema kuwa imewadia kwa wakati unaofaa.

“Kishutu ni hatua kubwa kwa mwanamke wa Kilifi ambayo italeta mabadiliko yanayostahili katika jamii yetu kwani imekuwa ishara ya kukutambua,” akasema.

Alisema hatua hiyo inainua utalii katika eneo la Pwani.

Waziri wa Jinsia Aisha Jumwa (kulia) azungumza na Naibu Gavana wa Kilifi Kilifi Bi Flora Chibule walipohudhuria sherehe za vazi maarufu la Kishutu katika uwanja wa Karisa Maitha ulioko mjini Kilifi mnamo Ijumaa, Desemba 1, 2023. PICHA | MAUREEN ONGALA
  • Tags

You can share this post!

Wauzaji pombe ‘mwitu’ kuona cha mtema kuni

Maina Njenga ni mradi wa Gachagua kuzima umaarufu wa...

T L