• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Serikali yatoa Sh8.7 bilioni kusaidia familia maskini

Serikali yatoa Sh8.7 bilioni kusaidia familia maskini

Na WINNIE ONYANDO

SERIKALI imetoa Sh8.7 bilioni Jumatano chini ya mpango wa Inua Jamii kama msaada kwa familia zisizojiweza hasa katika nyakati hizi ngumu ya kiuchumi.

Katibu Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Jamii, Bw Nelson Marwa alisema kuwa pesa hizo zitawafikia waliojisajili katika program hiyo kuanzia wiki ijayo.

Katika taarifa kwa wanahabari, Bw Marwa alisema kuwa walengwa wa program hiyo watapokea Sh8,000 kama malipo ya miezi ya Machi, Aprili, Mai na Juni mwaka huu.

“Serikali pia imetoa ongezeko la Sh26.3 milioni kama malipo ya ziada kwa walengwa 12,054 chini ya mpango wa Lishe Bora,” taarifa ilisoma.

Program hiyo ya Inua Jamii inalenga kuwasaidia familia zilizo na watoto wenye miaka chini ya miwili, wajawazito na wamama wanaonyonyesha ambao tayari wamejisajili.

Kaunti kama vile Kitui, Kwale, Turkana, Marsabit na Pokot Magharibi ndio walengwa wa program hiyo.

Inua Jamii ni program iliyoundwa ili kuwapa msaada wazee (OPCT), mayatima (CT-OVC), walemavu (PWSD-CT) na maeneo yanayokumbwa na ukosefu wa chakula (HSNP).

Lengo kuu la Inua Jamii ni kuimarisha hali ya maisha ya wasiojiweza kwa kuwapa misaada ya pesa kila mwezi.

You can share this post!

Huenda Guardiola akose kizibo cha Aguero

Aliyekuwa mchezaji wa Harambee Stars aendelea kutatizika...