• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Shule kufunguliwa Januari 8, 2024   

Shule kufunguliwa Januari 8, 2024  

NA SAMMY WAWERU 

KALENDA ya masomo itarejelea kama ilivyokuwa hapo awali, mwaka ujao, 2024, baada ya taifa na ulimwengu kukabili kikamilifu ugonjwa wa Covid-19.

Ratiba ya masomo nchini, ilikuwa imeathirika pakubwa Covid ilipotua.

Ugonjwa huo ambao ulikuwa janga la kimataifa uliosababishwa na virusi vya Corona, hata hivyo, haupo.

Akihutubu wakati wa utoaji rasmi wa Mtihani wa Kitaifa Darasa la Nane (KCPE) 2023, Katibu katika Wizara ya Elimu, Belio Kipsang alisema Alhamisi, Novemba 23, 2023 kwamba shule zitafunguliwa Januari 8, 2024 na hivyo basi kuwezesha kalenda ya masomo kurejelea kama ilivyokuwa hapo awali.

“Kuanzia mwaka ujao, 2024 kalenda ya masomo nchini itarejelea kama ilivyokuwa awali,” Dkt Kipsang akasema.

Matokeo ya KCPE 2023 yanatangazwa leo, Alhamisi, Novemba 23 na Waziri wa Elimu, Bw Ezekiel Machogu, Mitihani House, Jijini Nairobi.

“Ninapongeza waalimu kwa kazi nzuri waliyofanya wakati taifa lilikuwa linahangaishwa na Covid-19. Kwa mfano, mwaka uliopita, 2022, walipambana na mihula miwili ya masomo,” Katibu Kipsang akasema.

Matokeo ya KCPE 2023, yanafunga jamvi la mfumo wa 8-4-4 ulioanza 1985, na kubisha hodi mfumo mpya wa CBC.

Aidha, watahiniwa milioni 1.4 walifanya KCPE mwaka huu, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamke asimulia alivyoponyoka na wanawe mauti Shakahola...

Soko la Muthurwa ni chafu na limejaa tope, wafanyabiashara...

T L