• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
Shule ziboreshwe ili kuepusha ushindani mkali uliopo kwa sasa

Shule ziboreshwe ili kuepusha ushindani mkali uliopo kwa sasa

Na FRANKLIN MUKEMBUKAJUKI-NITHI

BAADA ya uteuzi wa wanafunzi wa darasa la nane wanaojiunga na Kidato cha Kwanza kuanzia Agosti, kumekuwa na malalamishi miongoni mwa wazazi, walezi na hata wanafunzi wengine wakidai hawakupewa nafasi katika shule walizozichagua.

Ukweli ni kwamba, sio rahisi wanafunzi wote kupata nafasi katika shule walizozichagua. Wanafunzi wangependa shule fulani kuliko nyingine lakini Wizara ya Elimu ilijaribu kusawazisha uteuzi huo ili wanafunzi kote nchini wanufaike.

Itakuwa vyema wadau wa elimu wahakikishe miundo msingi katika shule zetu imeboreshwa ili kuwavutia wasomi, wazazi na walezi ndipo tuweze kujivunia kuwapeleka watoto wetu.Kila mzazi angependelea mtoto wake ajiunge na shule maarufu nchini lakini hili haliwezekani kwa kuwa wanafunzi wanaofanya KCPE nao ni wengi mno.

  • Tags

You can share this post!

Serikali yanyenyekea kuhusu amri kwa makanisa

Kundi la Malenga Wamilisi na Kiswahili ni chanda na pete