• Nairobi
  • Last Updated May 24th, 2024 2:08 PM
Tanzania kuanza zoezi la utoaji chanjo dhidi ya gonjwa la corona

Tanzania kuanza zoezi la utoaji chanjo dhidi ya gonjwa la corona

Na CITIZEN

TANZANIA inajiandaa kuanza shughuli ya utoaji chanjo ya Covid-19 baada ya jopo la wataalamu kuwasilisha ripoti inayotoa mwongozo wa jinsi zoezi hilo litaendeshwa.

Kabla ya kifo cha aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli, Tanzania ilikataa kuagiza aina zozote za chanjo ya ugonjwa huo ikitilia shaka usalama wazo.Lakini mnamo Aprili Rais Samia Suluhu Hassan alibuni kamati ya wataalamu kuchunguza hali ya janga la Covid-19 nchini humo na kutoa mwelekeo kuhusu namna ya kukabiliana nalo.

Miongoni mwa mapendekezo mengine, kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Said Aboud ilipendekeza kwa serikali ilitoa nafasi kwa watu kupewa chanjo kwa hiari na serikali irejelee mtindo wa kutoa takwimu kuhusu idadi ya maambukizi kila siku.

Mnamo Jumamosi, jopo hilo liliwasilisha ripoti nyingine inayoelezea jinsi Tanzania inaweza kupata rasilimali za kutumia katika mpango wa kudhibiti msambao wa Covid-19. Vile vile, ripoti hiyo iliwasilishwa kwa Rais Suluhu, ilisheheni mkakati wa utoaji chanjo.

“Kamati hiyo ilishauri kwa fedha zitafutwa kimataifa na kutoka kwa sekta ya kibinafsi ili kufadhili mpango wa ununuzi vifaa, utoaji mafunzo na ununuzi wa chanjo,” akasema msemaji wa Afisi ya Rais Gerson Msigwa.

Hayo yalijiri siku moja baada ya Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kumwambia mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania Dkt Tigest Ketsela Mengistu kwamba kisiwa hicho kiko tayari kupokea chanjo ya Covid-19 na misaada mingine ya kupambana na janga hilo.

You can share this post!

Tanzania kuanza zoezi la utoaji chanjo dhidi ya gonjwa la...

TAHARIRI: Uteuzi wa majaji unatiliwa shaka