• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Tunatathmini mashtaka ya kumfungulia Mackenzie – Haji

Tunatathmini mashtaka ya kumfungulia Mackenzie – Haji

NA ALEX KALAMA

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) humu nchini Noordin Haji amesema ofisi yake inatathmini mashtaka ya kumfungulia mhubiri tata wa kanisa la Good News International Paul Mackenzie ikiwa ni pamoja na la ugaidi.

Kulingana na Haji, hatua hiyo itaipa idara hiyo muda wa kutosha kukamilisha uchunguzi na kupata ushahidi wa kutosha kuhusu madai yanayomkabili.

Akihutubia wanahabari katika eneo la Shakahola kwenye Kaunti ya Kilifi Haji aidha ameiomba idara ya mahakama kushirikiana nao ili watekeleze uchunguzi ipasavyo.

“Yale yaliyotokea hapa niyakusikitisha sana na tayari ni  kitu ambacho hatukutarajiwa kutokea katika nchi yetu. Tumeona umbali wa mahali hapa na ni msituni nadhani ndiyo sababu aliyetekeleza maovu haya alifanya hivi mahali ambapo anajua sio rahisi mtu kufikiria hali hii inaweza kutokea,” alisema Bw Haji.

Hata hivyo Bw Haji alidokeza kuwa inabidi wakae chini kama waendesha mashtaka ili kujadili na kushauriana juu ya aina gani ya mashtaka wangependelea aweze kushtakiwa nayo.

“Lakini kwa kuanzia, tunaangalia mashtaka ambayo kwa kweli tunawaadhibu watu waliohusika katika kanuni hii ya adhabu hayatoshi, bali tunaangalia na kuona ni aina gani ya ushahidi tunaoupata ili kuweza kuruhusu kumfungulia mashtaka katika mahakama,” alisema Bw Haji.

Aidha alibainisha kuwa yaliyotokea Shakahola yamesikitisha umma na akasisitiza watafanya wawezalo kuhakikisha kuwa anakabiliwa na mashtaka yanayoendana na maovu hayo.

“Mahakama ituunge mkono katika hili kwani wakati mwingine alipofikishwa mahakamani alipewa dhamana ya 10,000 tu. Na akarudi hapa na kuendelea kufanya alichokuwa anafanya. Hii haikubaliki kabisa. Kwa hivyo natumai tukienda mahakamani wataweza kutoa muda kwani idadi ya siku tunazohitaji ni siku nyingi ili kuweza kuchana ekari 800 za shamba hili na kuhakikisha hakuna miili iliyoachwa,” alisema Bw Haji.

DPP Noordin Haji akiwa katika msitu wa Shakahola. PICHA | WACHIRA MWANGI
  • Tags

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Tahadhari minyoo huathiri wakubwa kwa wadogo

Vifo: Serikali yaamka

T L