• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Uchumi uko sawa mpuuzeni Raila, Ruto aambia Wakenya

Uchumi uko sawa mpuuzeni Raila, Ruto aambia Wakenya

RAIS William Ruto ametetea mpango wa kuagiza mafuta ulioidhinishwa na serikali akisema ni chaguo bora zaidi kwa nchi, akizua majibizano mapya na kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga.

Dkt Ruto alieleza kuwa ndiye anayesimamia ufufuaji wa uchumi nchini na kwamba hivi karibuni utakuwa thabiti baada ya mwaka mzima wa misukosuko.

Rais pia alisema hatachukua mtazamo wa watu wengi katika kurekebisha uchumi kwani kuna haja ya kukabiliana na changamoto hizo moja kwa moja na kuzirekebisha.

“Nilijitolea kubadili mtindo wa uchumi wa nchi hii na kuondoa madeni tuliyokuwa tukihangaika nayo. Nina furaha kwamba sasa tumebadilisha mambo. Kenya inaenda vizuri kiuchumi,” Dkt Ruto alisema.

Akimjibu moja kwa moja Bw Raila kuhusu madai kwamba mpango huo utangazwe hadharani, Dkt Ruto alisema maelezo hayo tayari yamewasilishwa bungeni na yanapatikana na yeyote anayevutiwa nayo.

Bw Raila alitoa changamoto kwa serikali kuweka hadharani biashara hiyo aliyodai si ya Serikali-kwa-Serikali kama ilivyoelezwa awali, lakini ilikusudiwa kusamehe kampuni tatu za humu nchini – Gulf Energy, Galana Oil Kenya Limited na Oryx Energies Kenya – asilimia 30 ya ushuru wa kampuni.

  • Tags

You can share this post!

Jombi pabaya kwa kudai mvua ya mafuriko ni adhabu ya Mungu

Ndege mbili za helikopta zahusika katika ajali tofauti Wajir

T L