• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 9:59 AM
Ufisadi, ulafi vinasababisha majumba kuporomoka

Ufisadi, ulafi vinasababisha majumba kuporomoka

Na MARY WAMBUI

UFISADI miongoni mwa maafisa wa idara zinazosimamia ujenzi barabarani na wafanyabiashara walafi wanachangia katika ongezeko la majengo yanayoporomoka nchini.

Kulingana na utafiti uliofanywa, baadhi ya majengo si thabiti, jambo linaloweka maisha ya wanaoishi kwenye majengo hayo hatarini. Visa vya kuporomoka kwa majengo vya hapo awali vinaonyesha kuwa baadhi ya kesi hizo hazichunguzwi na wanakandarasi husika kukamatwa.

Kesi nyingi za awali hazina rekodi ya wazi ya hatua zilizochukuliwa, na kwa wachache ambao walifikishwa kortini, hawakuchukuliwa hatua yoyote na serikali. Watafiti sasa wanahusisha ongezeko kwa idadi za majengo yanayoporomoka na kuzembea kwa korti au maafisa husika katika kuangazia kesi hizo.

Mnamo 2016, Dorkami House na Neighbors Heights, zote za Juja, zilitangazwa kuwa ni hatari kwa umma baada ya madai ya kupasuka kwa ukuta na sakafu. Mmiliki wa majengo hayo, Robert Kamau Kamiti, alishtakiwa na serikali ya Kaunti ya Kiambu kwa kutekeleza maendeleo bila mpango ulioidhinishwa wa Dorkami, na kwa kukosa kujenga mtaa wa Neighbors Heights kulingana na mpango ulioidhinishwa.

Hata hivyo, hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na korti kuhusiana na kesi hiyo. Mnamo Oktoba 2009, jengo la orofa tano lililokuwa likijengwa katika mji wa Kiambu liliporomoka, na kuwauwa watu 17. Hakuna aliyekamatwa kutokana na ajali hiyo.

You can share this post!

IEBC huru kuandaa uchaguzi- Korti

Kijana mwenye vipaji vingi, anayevitumia kuwafaa wenzake

T L