• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
‘Ukosefu wa maji shuleni ni kikwazo kwa juhudi za kukabiliana na Covid-19’

‘Ukosefu wa maji shuleni ni kikwazo kwa juhudi za kukabiliana na Covid-19’

Na LAWRENCE ONGARO

IMEBAINIKA wazi ya kwamba shule nyingi za msingi katika eneo la Thika na vitongoji vyake zinazotegemea kampuni ya maji ya THIWASCO zimepata bili ya maji ya kiwango cha juu ajabu huku zikikatiwa maji yao.

Mwalimu mkuu wa Kenyatta Primary iliyoko mjini Thika Bw Francis Nyoike Chege, alisema shule yake ilipokea malimbikizo ya bili ya maji ya takribani Sh1.2 milioni kwa miezi kadha jambo ambalo linaponza juhudi zake za kupambana na homa ya Covid-19.

Alisema upungufu wa maji unaikabili shule hiyo.

Alizidi kueleza kuwa idadi ya wanafunzi walioko katika shule hiyo ni 1,940 na shule hiyo inahitaji maji mengi ya matumizi.

Bw Chege alipongeza juhudi za mbunge wa Thika za kusambaza matangi ya maji kwa shule za msingi 36 katika eneo lote la Thika.

Alisema tangi moja lina uwezo wa kuhifadhi maji lita 10,000 kwa wakati mmoja.

Bi Lydia Wambui ambaye ni mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiboko mjini Thika, alisema pia yeye anapitia masaibu hayo ya bili ya maji.

Alieleza bili yake ilikuja juu ambapo ni zaidi ya Sh1.5 milioni.

Alisema juhudi za kuwekwa tangi la maji kwa kila shule ni hatua nzuru ya kuhifadhi maji hasa wakati kunaponyesha mvua.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Barracks mjini Thika Bw John Kiarie, alisema wakati wa janga la Covid-19 shule nyingi mjini Thika zilipata shida sana kutokana na ukosefu wa maji ya matumizi.

“Hata hivyo, matangi tunayoletewa na mbunge wetu wa Thika ni muhimu sana kwa kuhifadhi maji ya kutumiwa na wanafunzi,” alisema Bw Kiarie.

Mbunge wa Thika Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina, alisema mpango huo wa kusambaza matangi kwenye shule za msingi ni muhimu hasa wakati huu wa janga la Covid-19.

“Mpango huo ni kupitia fedha za maendeleo za NG-CDF, na umekuwa wa kufana. Tukianza mwakani, tutazuru shule zote hizo tukisambaza matangi hayo,” alifafanua mbunge huyo.

Hata shule hizo alieleza kuwa baada ya kufanyiwa ukarabati madarasa kadha yamerejea kuwa ‘mapya’ huku wanafunzi na walimu wakipata motisha katika mazingira mapya.

  • Tags

You can share this post!

Leads United, Patriots Queens, Shule ya Farasi Lane na...

Amri meli yenye vifaa hatari itengwe

T L