• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:55 PM
Vyama tayari kuvuna kupitia mchujo

Vyama tayari kuvuna kupitia mchujo

NA ONYANGO K’ONYANGO

VYAMA vya kisiasa vinatarajiwa kuvuna mamilioni ya pesa kutoka kwa wawaniaji wanaopanga kuwania nyadhifa mbalimbali za kisiasa shughuli za mchujo zinapokaribia.

Huku kampeni za uchaguzi wa Agosti zikianza kushika kasi, vyama vingi vimejiweka tayari kupokea fedha hizo, wawaniaji wanap – ong’ang’ania tiketi zake.

Katika nafasi za udiwani, karibu kila chama kinalenga kupata Sh81.2 milioni. Kuna nafasi 1,881 za udiwani nchini.

Katika nafasi za ugavana, vinalenga kupata Sh23.5 milioni, huku nafasi za useneta, uwakilishi wa wanawake na ubunge zikitarajiwa kuvizolea Sh11.8 milioni, Sh9.4 miliomi na Sh72.5 milioni mtawalia.

Kiasi hicho ni ikiwa chama kitafanikiwa kupata ombi kwa mwaniaji kutoka kila nafasi ya kisiasa.

Kama ishara ya ushindani mkubwa utakaokuwepo kwenye shughuli hizo, Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa imepokea zaidi ya maombi 1,000 ya usajili wa vyama vya kisiasa tangu 2017. Tayari, vyama vitano vya kisiasa—United Democratic Alliance (UDA), Amani National Congress

(ANC), Ford-Kenya, Chama Cha Kazi na United Party of Independence Alliance (UPIA)—vishaanza mikakati ya kuendesha zoezi hilo.

Vyama vingine vinatarajiwa kutangaza mikakati yake wiki chache zijazo.

Mnamo 2017, jumla ya wawaniaji 12, 119 walishiriki kwenye shughuli za mchujo. Wadadisi wasema huenda idadi ya wawaniaji ikaongezeka mara hii. Katika kile kinachoonekana kama mkakati wa kuwavutia wanawake zaidi kuwania nyadhifa tofauti za kisiasa, vyama vingi vimepunguza ada ambazo wanawake wanahitajika kulipa ili kushiriki kwenye mchujo.

Vingi vimepunguza ada hizo kwa asilimia 50 kwa wanawake na vijana. Walemavu hawatakuwa wakilipa ada zozote katika vyama vya UDA, CCK na UPIA. Katika chama cha UDA, ambacho kinaongozwa na Naibu Rais William Ruto, wawaniaji wamepewa hadi mwishoni mwa mwezi huu kutuma maombi yao.

“Maombi hayo yanapaswa kutumwa kupitia tovuti ya chama,” akaeleza mwenyekiti wa chama hicho, Bw Anthony Mwaura.

Wawaniaji wanaolenga kuwania ugavana watalazimika kulipa Sh500,000 kama ada za mchujo, huku wabunge wakitozwa Sh250,000.

Madiwani watalipa ada ya Sh50,000. Katibu Mkuu wa chama hicho, Bi Veronicah Maina, alisema hawatakuwa na mapendeleo yoyote.

“Hakuna wawaniaji wanaopendelewa. Shughuli zote zitaendeshwa kwa njia ya wazi,” akasema.

Majuzi, Dkt Ruto alisisitiza kuhusu haja ya uwepo wa michujo itakayoendeshwa kwa njia ya uwazi na haki.

  • Tags

You can share this post!

Siri ya mawaziri ‘wanasiasa’ kutojiuzulu viti

Nicole: Talanta yangu ipo kwenye damu

T L