• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Wabunge wahimiza wazazi walinde watoto wao

Wabunge wahimiza wazazi walinde watoto wao

NA MWANDISHI WETU

MBUNGE wa Lunga Lunga Khatib Mwashetani (pichani) na mwenzake wa Jomvu Bw Badi Twalib wamewasihi wazazi kuwalinda watoto wao baada ya shule kufungwa kwa muhula wa kwanza.

Bw Twalib alilalamika kuwa watoto wanaonekana wakiranda randa mitaani kuhatarisha maisha yao akiwataka wazazi kuwa makini na watoto wao baada ya kufunga shule.

“Kazi ya wanafunzi ni kusoma si kupiga magwaride. Msitumie watoto kupiga magwaride, shule zimefungwa wanafunzi waendelee kusoma hata kama waende masomo ya ziada ni sawa,” alisema Bw Twalib kwenye kampeni huko Jomvu.

Bw Mwashetani ambaye aliongea kwenye hafla ya kuwazawadi wanafunzi wa shule ya msingi ya Kikoneni aliwasihi wanafunzi watie bidii masomoni.

“Walimu wanafanya kazi ngumu sana kwa sababu yao ni taaluma ya kujitolea na hakuna mtu anaweza kuwalipa kiasi chao,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Ombi la Nyong’o kuendelea kuishi kwa nyumba ghali lazua...

Kipa Dean Henderson aondoka Man-United na kujiunga na...

T L