• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Kipa Dean Henderson aondoka Man-United na kujiunga na Nottingham Forest kwa mkopo

Kipa Dean Henderson aondoka Man-United na kujiunga na Nottingham Forest kwa mkopo

Na MASHIRIKA

LIMBUKENI wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Nottingham Forest, wamemsajili kipa Dean Henderson wa Manchester United kwa mkopo.

Henderson, 25, alikuwa na hamu ya kugura uga wa Old Trafford baada ya David de Gea kufanywa kipa chaguo la kwanza kambini mwa Man-United.

“Ana kiu ya kuwajibishwa mara kwa mara katika kikosi cha kwanza,” akasema kocha wa Forest, Steve Cooper.

Henderson anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Forest baada ya fowadi mzoefu raia wa Nigeria, Taiwo Awoniyi aliyetokea kambini mwa Union Berlin.

Henderson anajivunia rekodi ya kutofungwa bao katika 17 kati ya 49 kwenye kipute cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Hata hivyo, hajawahi kuwajibishwa katika pambano lolote la EPL tangu Mei 2021.

Henderson ambaye amewajibishwa na Uingereza mara moja pekee tangu mwaka wa 2020, analenga kuwa sehemu ya kikosi kitakachotegemewa na kocha Gareth Southgate kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia mnamo 2022 nchini Qatar.

Brice Samba amekuwa kipa chaguo la kwanza la Forest katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita. Mlinda-lango huyo mwenye umri wa miaka 28 angali na mkataba na Forest hadi mwaka wa 2023 japo juhudi za kumshawishi arefushe kandarasi yake bado hazijazaa matunda.

Forest ambao wamerejea kushiriki EPL kwa mara ya kwanza tangu 1999, wameratibiwa kufungua kampeni zao za msimu ujao wa 2022-23 dhidi ya Newcastle United mnamo Agosti 6, 2022.

Forest wanahusishwa pakubwa na beki raia wa Ufaransa, Giulian Biancone, 22, kutoka Troyes wanaoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wabunge wahimiza wazazi walinde watoto wao

Everton wasajili difenda James Tarkowski kutoka Burnley...

T L