• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Wadi Nairobi isiyo na hospitali wala shule ya umma

Wadi Nairobi isiyo na hospitali wala shule ya umma

NA WINNIE ONYANDO

DIWANI (MCA) wa Lindi katika Kaunti ya Nairobi Samson Ochieng Jera amethibitisha kuwa wadi yake haina hospitali, shule wala soko la umma.

Akizungumza na Taifa Leo, diwani huyo ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa chama cha ODM tawi la Nairobi, alisema kuwa kwa sasa analenga kujenga hospitali ya Level 2 katika wadi yake.

“Hii ndiyo wadi Nairobi ambayo haina shule, hospitali na soko la umma. Baadhi ya watu katika eneo hili wanalazimika kutafuta huduma za matibabu katika wadi nyingine. Hii ni changamoto sana kwetu,” akasema Bw Jera.

Kwa upande mwingine, alisema kuwa nguvu za umeme zinasumbua sana katika eneo hilo.

“Hii imefanya visa vya uwizi kuongezeka maradufu katika eneo hili. Vijana sasa wanatumia nafasi hiyo kuwaibia wafanyabiashara barabarani,” akaongeza Bw Jera.

Kadhalika, alilalamika kuwa wadi hiyo haijawahi kuwa na ofisi ya diwani.

“Mimi ndiye diwani wa kwanza kujenga ofisi ya diwani. Kwa sasa, wakazi wanaweza kuja katika ofisi yangu hapa na kupata huduma,” akaongeza Bw Jera.

Kuna wakati ambapo wakazi walikuwa wanalazimika kwenda nyumbani kwa diwani wa zamani.

  • Tags

You can share this post!

Madereva wa masafa marefu wakataa kurudi darasani

Faida ya madini hatujaiona kikamilifu Kwale – Wakazi

T L