• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Wafugaji watishia kususia misaada wasipopewa pia lishe ya mifugo yao

Wafugaji watishia kususia misaada wasipopewa pia lishe ya mifugo yao

Na KALUME KAZUNGU

JAMII za wafugaji katika maeneo ya Pwani zimeitaka serikali iharakishe kutuma lishe ya msaada kwa mifugo yao, huku idadi ya mifugo inayofariki kwa sababu ya njaa ikiendelea kuongezeka.

Katika Kaunti ya Lamu, wafugaji wametishia kususia chakula cha msaada kwa binadamu wanachopewa ikiwa serikali ya Kaunti na wahisani hawatasaidia mifugo yao.

Gavana wa Lamu, Bw Fahim Twaha alizindua usambazaji chakula cha msaada kwa wakazi walioathirika na ukame wiki iliyopita, hasa unga wa mahindi.

Mwenyekiti wa Muungano wa Kitaifa wa Soko la Mifugo, tawi la Lamu, Bw Khalif Hiribae, alisema hawajafurahia jinsi serikali ya kaunti na wahisani wanavyoshughulikia athari za ukame eneo hilo.

Zaidi ya mifugo 500 imeripotiwa kufariki katika maeneo mbalimbali Lamu tangu athari za ukame zilipoanza kuathiri nchi.

“Hatufurahi kwamba binadamu wanapewa misaada ilhali mifugo yetu ikiachwa kuangamia kwa njaa na ukosefu wa maji. Wakitaka kutusaidia basi walete vyakula vya binadamu na mifugo. Ikiwa hilo hawaliwezi, basi wabaki na misaada yao. Waache sisi na mifugo yetu tuangamie sote,” akasema Bw Hirbae.

You can share this post!

Wanasiasa wabuni njama IEBC ikisajili wapigakura wapya

WANGARI: Mikakati yahitajika kupunguza mzigo wa matibabu...