• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Wakenya waelezea kumkosa Rais Mstaafu Kenyatta huku wakiadhimisha bethidei yake

Wakenya waelezea kumkosa Rais Mstaafu Kenyatta huku wakiadhimisha bethidei yake

NA MERCY KOSKEI

RAIS mstaafu Uhuru Muigai Kenyatta leo Oktoba 26, 2023 anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kuadhimisha miaka 62.

Hata hivyo, Wakenya wameelezea kumkosa Bw Kenyatta huku wakiadhimisha bethidei yake.

Wakenya walifurika kwenye mtandao ya kijamii ya Twitter kumtakia heri njema ya kuzaliwa.

Steve Khari “Heri njema ya kuzaliwa Bwana Rais.”

Michael Onimbo “Heri njema ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta.”

Luis Official: “Heri njema ya kuzaliwa Bwana Rais. Furahia siku yako.”

Kiunge Njenga:”Heri njema ya kuzaliwa kwa Rais mwema nchi ya Kenya ishawai kuwa nayo.”

Uhuru ni rais wa nne wa Kenya aliyehudumu kwa mihula miwili kuanzia 2013 hadi 2022.

Ni mtoto wa Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya. Akiwa mtoto, Uhuru aliandamana na babake kwenye hafla nyingi za umma.

Amemuoa Margaret Kenyatta. Walifunga ndoa mnamo 1991. Wana watoto watatu: Jomo, Muhoho na Ngina.

  • Tags

You can share this post!

Mbio za Standard Chartered Nairobi Marathon zavutia...

Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa yachapisha video kuonyesha...

T L