• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:17 PM
Wakulima walalamikia kanuni mpya za miwa

Wakulima walalamikia kanuni mpya za miwa

Na RUTH MBULA

WAKULIMA wa miwa eneo la Trans Mara wamepinga kanuni mpya zilizoanzishwa na kampuni ya sukari ya Trans Mara, ya kutovuna miwa iliyoteketezwa na moto shambani.

Wakisema kanuni hizo ni dhalimu walimtaka Waziri wa Kilimo Peter Munya kuingilia kati suala hilo, licha ya kampuni ya Trans Mara kutetea uamuzi huo ikisema itaikinga dhidi ya hasara.

“Kuanzia sasa hatutavuna na kusafirisha miwa iliyoteketezwa ikiwa shambani,” ilisema ilani iliyotiwa saini na Afisa Mkuu Mtendaji wa Trans Mara, Bw Frederick North Coombes.

Kuambatana na kanuni hizo mpya, mkulima anaweza kuvuna miwa yake na kuisafirisha lakini atatozwa ada fulani.

Vile vile, akifeli kusafirisha zao hilo hadi kiwandani, bado atatozwa ada ya adhabu.Bw North alisema uamuzi huo ulitokana na ongezeko la visa vya miwa kuteketezwa eneo hilo la Trans Mara, ambapo kufikia sasa jumla ya 431 vimeripotiwa.

Miwa hiyo, alieleza, huathiri ubora wa sukari inayozalishwa baada ya zao hilo kusagwa.“Kanuni hizi mpya zimeanzishwa baada ya zile za awali kukosa kuzuia visa vya uteketezaji wa miwa,” akasema Bw North.

Mwezi Machi kampuni ya Trans Mara Sugar pia ilianzisha kanuni zingine kuhusu ukataji na usafirishaji wa miwa, kanuni ambazo kufikia sasa hazijaanza kutekelezwa.

Hata hivyo, wakulima walisema kuwa wanaunga mkono kanuni hizo za Machi ila wanapinga mpya za sasa kuhusu usafirishaji wa miwa iliyoteketezwa.

Chini ya kanuni za awali, kampuni ilikuwa ikitoza ada ya Sh400 kwa kila tani ya miwa iliyoteketea. Vile vile, kulikuwa na ada zingine kuhusiana na thamani ya miwa.Aidha, kampuni ilikuwa ikikata ada ya kufidia bei ya pembejeo za miwa iliyoteketezwa, kando na kucheleweshwa kwa malipo ya wakulima kwa miezi mitatu.

“Wakulima wanaumia, tunaomba kampuni iondoe kanuni hizi kandamizi,” alisema Mweka Hazina wa Shirikisho la Kitaifa la Wakulima wa Miwa (KNFSF), Stephen Ole Narupa, mnamo Jumamosi.

Ole Narupa akakariri.Mnamo Jumamosi Mweka Hazina wa Shirikisho la Kitaifa la Wakulima wa Miwa (KNFSF) Stephen Ole Narupa alisema kanuni hizo mpya ni dhalimu kwa sababu visa vya miwa kuteketea huwa ni ajali.

“Wakulima hawafai kuadhibiwa kutokana na kuteketea kwa miwa ilhali visa hivi huwa ni ajali ambayo yamkini haiwezi kuepukika,” akaeleza.

“Wakulima wetu wanaumia na tunaomba kampuni ya sukari ya Trans Mara kuondoa kanuni hizi kandamizi,” Ole Narupa akakariri.

You can share this post!

Viongozi wa kidini wasuta wanasiasa kupepeta corona

AFC Leopards youth yateleza ligi ya NWRL