• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Waliovamia wanahabari wamulikwa

Waliovamia wanahabari wamulikwa

NA MARY WANGARI

BARAZA la Vyombo vya Habari nchini (MCK) limeanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo wanahabari watatu walishambuliwa na maafisa wa serikali ya Kaunti ya Kilifi.

Bw Elias Yaa (gazeti la The Star), Daniel Peshu na Maureen Ongala (Daily Nation) walishambuliwa Ijumaa na watu wanaodaiwa kutoka afisi ya gavana wa kaunti hiyo. Walikuwa wanaangazia maandamano dhidi ya Gavana katika uwanja wa Karisa Maitha.

Kisa hicho kinachohusu waajiriwa waliokuwa wameandamana na Mkuu wa Wafanyakazi katika Kaunti kimeripotiwa katika Kituo cha Polisi kwenye nambari ya OB 33/23/12/2023.

“MCK ingependa kufahamisha waliohusika na umma kuwa mashambulizi yoyote dhidi ya wanahabari ni kitendo cha uhalifu na ni kinyume cha haki za wanahabari,” ilisema MCK kupitia taarifa.

  • Tags

You can share this post!

KIGODA CHA PWANI: Uchaguzi mkuu ulivyobadili mkondo wa...

Mswada wa kusuluhisha mvutano kuhusu upande wa walio wengi...

T L