• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 9:50 AM
Wamaasai wataka operesheni Laikipia isitishwe

Wamaasai wataka operesheni Laikipia isitishwe

Na RICHARD MUNGUTI

BARAZA la Jamii ya Maasai limewaliwasilisha kesi mahakama kuu likiomba operesheni ya maafisa wa usalama katika Kaunti ya Laikipia ikomeshwe mara moja.

Katika kesi iliyowasilishwa katika mahakama kuu na baraza hilo kupitia kwa mawakili Thomas Letangule ma Abdi Noor wafugaji wamepoteza zaidi ya ng’ombe 1,600 walio na thamani ya zaidi ya Sh160milioni.

Katika kesi hiyo, mahakama imeelezwa wafugaji wameuawa na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa.

Mahakama kuu imeelezwa wafugaji wasio na hatia wameathiriwa pakubwa kufuatia operesheni hiyo.

Wakiongozwa na wabunge wawili wa zamani David ole Sankori (Kajiado ya Kati) na Peter Stephen Lenges pamoja na mwenyekiti wa baraza hilo Bw Kelena ole Nchoe, wafugaji hao wanaomba korti isitishe oparesheni hiyo inayoendelezwa na maafisa wa polisi.

Wameeleza mahakama kuu haki za wafungaji zimekandamizwa na ng’ombe wao wamechukuliwa na maafisa wa usalama pasi na sababu.

Walalamishi hawa wamesema kuwa wafugaji wamenyanyaswa na mali zao kuporwa na maafisa wa usalama.

Bw Letangule amesema wafugaji wamefujwa mali zao na sasa wanasukumiwa hali ya uchochole badala ya serikali kuwasaidia kujistawisha.

Katika kesi hiyo wazee hao wanaomba mahakama iamuru serikali iweke mwongozo wa kuwezesha jamii ya waamasai kulisha mifugo wao popote palipo na nyasi.

You can share this post!

Watatu wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Lamu

Mang’u Youth FC yaendelea kuongoza ligi ya Kanda ya...