• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Wanafunzi 20,000 waahidiwa vitambulisho

Wanafunzi 20,000 waahidiwa vitambulisho

KNA na DPPS

SERIKALI imeanza mpango wa kutoa zaidi ya vitambulisho 20,000 kwa wanafunzi kote nchini, huku shughuli za kuwasajili wapigakura zikiingia siku ya tatu leo Jumatano.

Kwenye mpango huo utakaoendeshwa kwa siku 30, maafisa kutoka Idara ya Kusimamia Huduma za Umma katika Wizara ya Usalama wa Ndani, watakuwa wakienda katika shule mbalimbali za upili kote nchini kutoa vitambulisho hivyo kwa wanafunzi ambao wamefikisha umri wa miaka 18.

Kulingana na Msimamizi Mkuu wa Usajili wa Watu katika Kaunti ya Murang’a, Mugira Munene, shughuli hiyo itaendeshwa kati ya Oktoba 18 na Novemba 17.

Bw Munene alisema watakuwa wakiwasajili wanafunzi hao hata wikendi na Sikukuu.

“Wakati wa utekelezaji wa mpango huo, tunawalenga hata wale ambao hawajawahi kupewa vitambulisho hivyo,” akaongeza.

Idara hiyo inasema imewaandikia barua walimu wakuu wa shule za upili, kuwarai wanafunzi ambao wamefikisha umri huo kubeba vyeti vyao vya kuzaliwa na vitambulisho vya wazazi wao watakaporejea shuleni kuanzia Jumatatu ijayo.

You can share this post!

Idadi ndogo ya wanaojiandikisha wawe wapigakura yashuhudiwa...

Facebook yaomba radhi baada ya huduma kupotea