• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Wanakarate chipukizi wapandishwa gredi

Wanakarate chipukizi wapandishwa gredi

NA LAWRENCE ONGARO

WANAKARATE chipukizi wapatao 34 walipata gredi tofauti katika zoezi la kutambua ujuzi wao katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Verona mjini Thika.

Klabu ya Gojuryu Karate-Do Seiwakai Kenya, chini ya Mkufunzi Mkuu Martin Ndegwa iliendesha zoezi hilo lililojumuisha wavulana na wasichana.

Miongoni mwa wanakarate hao, wanne walipata mshipi wa hudhurungu, wanne walipata mshipi wa kijani kibichi, 10 waliridhika na mshipi wa rangi ya chungwa, halafu 16 walipata mshipi wa manjano.

Kulingana na kocha huyo, wanakarate hao ni wa umri ya kati ya miaka mitano na 11 kutoka shule za kibinafsi za Consolata School Academy (Kiambu) na Thika Brook Academy (Thika).

“Ni muhimu kukuza mchezo wa karate hasa kwa vijana chipukizi. Klabu yangu itafanya juhudi kuona ya kwamba vijana wanapata mafunzo kamili ya karate,” alifafanua mkufunzi Ndegwa.

Alisema hiyo ni mwanzo wa kuwakuza chipukizi hao ili wawe na nidhamu, waweze kujiamini, na pia kuwajenga kiafya.

Alisema wakati wa shule chipukizi hao hupewa muda wa siku moja ya wiki kufanya mazoezi ili pia waweze kujihusisha zaidi na masomo.

Hata hivyo, alisema wakati huu wa likizo klabu yake ya Gojuryu Karate-Do Seiwakai Kenya itaendesha mazoezi ya siku tatu kwa wiki katika mji wa Thika.

Ametoa wito kwa wazazi kufanya hima ili kuwapeleka wana wao kwenye mazoezi ya karate ili wawe watoto wa kutegemewa na umma siku zijazo.

Kocha huyo amesema mazoezi mengine ya kupandisha wanakarate wengine gredi yatafanyika Oktoba 2023.

Ametoa wito kwa wanakarate hao kuhakikisha wanaonyesha nidhamu wanapojunuika na wananchi.

“Nimewashauri wanakarate hao kuwa mchezo huo sio wa kujigamba nao bali ni ujuzi wa kushiriki michezoni na kujikinga dhidi ya adui,” alisema kocha huyo.

  • Tags

You can share this post!

NYOTA WA WIKI: Ollie Watkins

Pasta Mackenzie asema anafunga licha ya kuwa seli

T L