• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Washukiwa wa kashfa ya Anglo-Leasing Obure, Kyungu waachiliwa huru

Washukiwa wa kashfa ya Anglo-Leasing Obure, Kyungu waachiliwa huru

NA RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Chris Obure, na makatibu wawili wa zamani Sammy Kyungu na Samwel Chamobo Bundotich walioshtakiwa miaka saba iliyopita kuhusiana na kashfa ya Anglo Leasing, Ijumaa waliachiliwa huru.

Watatu hao waliachiliwa na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya kuamua kesi za ufisadi, Bi Ann Mwangi aliyesema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi kuwezesha korti kuwapata na hatia.

“Ingawa watatu hawa waliidhinisha malipo ya mamilioni ya pesa kugharimia miradi ya Anglo-Leasing, hawakujinufaisha na senti hata moja,” alisema Bi Mwangi.

Bi Mwangi alisema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi kuonyesha jinsi watatu hao walivyohusika katika kashfa hiyo ikitiliwa maanani aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Amos Wako aliidhinisha kandarasi za miradi 18 ya Anglo-Leasing.

Watatu hao walikuwa wameshtakiwa pamoja na aliyekuwa mkuu wa shirika la Posta, marehemu Francis Chahonyo.

Miradi iliyonuiwa kufadhiliwa na pesa hizo za Anglo-Leasing ilikuwa ya ujenzi wa maabara ya idara ya polisi iliyozinduliwa rasmi wiki hii na Rais Uhuru Kenyatta.

Maabara hiyo ya kufanikisha utenda kazi wa polisi ilijengwa katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI).

  • Tags

You can share this post!

Afisa wa afya aonya wakazi kuhusu corona, homa

Basketiboli: Moischers Nets yaiadhibu Baobab Blazers

T L