• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Wito Kenya Power itumie tariff maalum kwa kampuni za maji

Wito Kenya Power itumie tariff maalum kwa kampuni za maji

NA ALEX KALAMA

WABUNGE katika kaunti ya Kilifi wamepewa changamoto kupeleka mswada bungeni ili kuhakikisha kuwa kampuni ya umeme nchini inapeana kampuni za maji Tarrif za kipekee na kuepuka madeni makubwa ambayo yamekua yakisababisha kukatwa kwa moto na kukosesha wenyeji maji masafi kutoka kwa serikali za kaunti.

Akizungumza katika eneo bunge la Ganze Rashid Mohamed ambaye ndiye mwenyekiti wa kampuni inayosambaza maji Kilifi na Mariakani KIMAWASCO ameeleza kuwa kwa muda sasa wenyeji wamekua wakilazimika kupata maji siku chache za wiki kutokana na deni kubwa ambalo kampuni hiyo na kaunti ya Kilifi inadaiwa.

“Kampuni za maji zinashindwa na kazi ya kusambaza maji kwa sababu ya KPLC gharama iko juu kama sisi huku hatuna mvuto inabidi kupigwe mtambo ungurume ndio usukume maji kupeleka Kilifi.

Pelekeni bunge hoja angalau hizi kampuni za maji zipate ushuru maalum ili iweze kuwasaidia waezekuhimili,si kila siku mkurugenzi mkuu wa maji anaenda ofisi ya gavana tusaidie moto umekatwa,” alisema Bw Mohamed.

Aidha Mwenyekiti huyo vile vile amewaonya wenyeji dhidi ya kuvunja mifereji na kuiba vifaa muhimu vya maji na akawasihi kupiga ripoti kwa machifu na wazee wa mtaa iwapo watashuhudia yeyote akichukua hatua kama hizo.

“Ni sisi wenyewe tuweze kulinda pipu kama hii ikiwa kweli tuna shida na tunataka matatizo ya maji tuepuke. Na wale kwamba wanavuruga pengine baada ya kesho kutwa tukija utapata mfereji pale umevunjwa pipu imetobolewa watu wote wanaangalia serikali ya kaunti.

Ni sisi tulinde huu mradi na wale waizi ambao kwamba wanazitoboa zile pipu tuweze kuwa wazi tufikishe hizi habari kwa ofisi za machifu ili kulinda huu mradi,” alisema Bw Mohamed.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua aapa kutounga handisheki ya Ruto na Odinga

Waliofanya kazi ya IEBC kusubiri zaidi malipo yao ya Sh1.9bn

T L