• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
Wizara ya Kilimo inavyoshirikisha vijana na kuwapa motisha kuzamia kilimo

Wizara ya Kilimo inavyoshirikisha vijana na kuwapa motisha kuzamia kilimo

Na SAMMY WAWERU

WAZIRI msaidizi katika Wizara ya Kilimo, CAS Anne Nyaga amesema idara yake imeweka mikakati kabambe kushirikisha vijana katika shughuli za kilimo.

Bi Nyaga amesema kamati maalum ya vijana imebuniwa ili kutoa ushauri na maelekezo kwa Wizara ya Kilimo kuwapa vijana motisha kuingilia na kuendeleza kilimo.

“Kamati yenyewe ilizinduliwa Aprili 2021,” akasema. Alisema inahusisha idara tofauti katika Wizara ya Kilimo, na pia kushirikiana na wizara husika zingine. “Tayari imeanza kuchapa kazi, na inajukumika kutoa maoni na ushauri kwa wizara,” Bi Nyaga akaelezea, akizungumza jijini Nairobi.

Kauli ya CAS Nyaga imejiri baada ya shirika moja lisilo la kiserikali, Heifer International kutoa ripoti inayoashiria idadi ya chini ya vijana wanaofanya kilimo.

Kwa mujibu wa shirika hilo linaloangazia masuala ya kilimo na ufugaji, asilimia 59 ya vijana wanalalamikia kukosa ardhi kushiriki shughuli za kilimo. Nchi 11 kutoka Magharibi mwa Bara Afrika, Kusini na Afrika Mashariki zilishiriki katika utafiti huo, Kenya ikiwemo.

Bw George Odhiambo, Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International, tawi la Kenya…PICHA/ SAMMY WAWERU

Asilimia 38 ya vijana waliohojiwa walisema hawana fedha, 34 kukosa mafunzo kuendeleza kilimo, huku asilimia 11 wakisema hawana habari kuhusu mifumo ya teknolojia ya kisasa kuboresha shughuli za kilimo.

“Hali hiyo inawiana katika nchi zote zilizoshiriki utafiti, Kenya ikiwemo,” Bw George Odhiambo, Mkurugenzi Mkuu wa Heifer International, tawi la Kenya akasema.

Maoni hayo yalikusanywa kutoka kwa vijana 29, 954, wakulima wadogo na wa kadri 299 na kampuni na mashirika 110 ya kilimo-ufugaji.

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa Arsenal jeraha likimweka nje kiungo Granit Xhaka...

KANU yamteua Gideon Moi kuwania urais 2022