• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:42 PM
Kirinyaga kuzindua kiwanda cha kuongeza nyanya thamani

Kirinyaga kuzindua kiwanda cha kuongeza nyanya thamani

Na SAMMY WAWERU

KIRINYAGA ni miongoni mwa kaunti zinazozalisha zao la nyanya kwa wingi nchini.

Gavana wa kaunti hiyo, Anne Waiguru alisema hayo Jumatano wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Mashujaa kwamba kiwango kikubwa cha zao hilo huharibika na pia kuoza kwa sababu ya kero ya soko.

Kutokana na hasara hiyo kwa wakulima, Bi Waiguru alitangaza kwamba Kirinyaga itazindua kiwanda cha kuongeza nyanya thamani.

“Kwa mwaka, Kirinyaga huzalisha zaidi ya tani 60,000 na kiwango kikubwa huharibika na kuoza kwa sababu ya changamoto za upatikanaji wa soko,” akasema.

Akaongeza: “Ni kwa sababu ya hasara wanayokadiria wakulima tumeweka mikakati kabambe kuwanusuru na hivi karibuni tutazindua kiwanda cha kuongeza nyanya thamani.”

Bi Waiguru hata hivyo hakufichua thamani ya kiwanda hicho, kifedha.

Nyanya ni kati ya mazao mabichi ya shambani ambayo soko lake limevamiwa na madalali, mawakala ambao wanalaumiwa kuchangia bei kuwa duni.

Kirinyaga ndiyo ilikuwa mwenyeji wa sherehe za Mashujaa Dei 2021

You can share this post!

Waiguru asifu Ajenda Kuu Nne za Rais Kenyatta akisema...

Kipchoge kuwania tuzo ya mwanariadha bora duniani dhidi ya...

T L