• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Kipchoge kuwania tuzo ya mwanariadha bora duniani dhidi ya Cheptegei, wengine wanane

Kipchoge kuwania tuzo ya mwanariadha bora duniani dhidi ya Cheptegei, wengine wanane

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA mara mbili wa marathon kwenye Olimpiki, Eliud Kipchoge ana fursa nyingine ya kuwania tuzo ya mwanariadha bora duniani.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo bora duniani mwaka 2018 na 2019 kutiwa Alhamisi katika orodha ya wawanizi wa tuzo ya mwanariadha bora dunia mwaka 2021.

Shirikisho la Riadha Duniani (WA) limetangaza majina ya wanariadha 10 wataoawania tuzo hiyo ya kifahari itakayopeanwa mwezi Desemba 2021.

Kipchoge ameshinda mashindano yake mawili ameshiriki mwaka huu – NN Mission Marathon katika uwanja wa ndege wa Twente mjini Enschede, Uholanzi mwezi Aprili na Olimpiki mjini Sapporo nchini Japan.

Gunge huyo, ambaye atafikisha umri wa miaka 37 hapo Novemba 5, anawania tuzo hiyo dhidi ya bingwa wa Olimpiki mbio za mita 5,000 Joshua Cheptegei (Uganda), mshindi wa Olimpiki na Diamond League wa kurusha tufe Ryan Crouser (Amerika), mfalme wa Olimpiki, Diamond League na Bara Ulaya kuruka kwa kutumia fito Mondo Duplantis (Uswidi), na mshikilizi wa rekodi za Ulaya mbio za mita 1,500 na mita 5,000 Jakob Ingebrigtsen (Norway) ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki mbio za mitya 1,500 na bingwa wa mbio za mita 1,500 za Ukumbini barani Ulaya.

Pia, kuna gunge wa “Triple Jump” Daniel Stahl (Uswidi), Mgiriki Miltiadis Tentoglou (Long Jump), raia wa Canada Damian Warner (Decathlon) na bingwa wa Olimpiki na Diamond League mbio za mita 400 kuruka viunzi Karsten Warholm (Norway).

Wawanizi hao watapigiwa kura kwa njia tatu kuamua mshindi. Baraza la Shirikisho la Riadha Duniani na familia ya shirikisho hilo zitatuma kura zao kupitia baruapepe, nao mashabiki watapiga kura kwenye mitandao ya jamii ya Shirikisho la Riadha Duniani.

Kura za Baraza zitajumuisha asilimia 50, familia ya WA asilimia 25 na mashabiki asilimia 25. Upigaji wa kura utafungwa Novemba 6. Orodha ya wawanizi kinadada utatangazwa Oktoba 22. Mwisho wa shughuli ya kupiga kura, wanaume watano na idadi sawa ya kinadada watatangazwa na WA kusalia mbioni kutawazwa washindi watakaojulikana mwezi Desemba.

You can share this post!

Kirinyaga kuzindua kiwanda cha kuongeza nyanya thamani

Afueni kwa wamiliki wa baa na hoteli

T L