• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Mbunge afurahia hatua ya vijana kuacha pombe

Mbunge afurahia hatua ya vijana kuacha pombe

NA LAWRENCE ONGARO

KUNA ya kuhakikisha vijana walioasi pombe na kujirekebisha wanapata mawaidha ili wapate dira bora ya maisha.

Vijana wapatao 100 kutoka kijiji cha Makwa, Gatundu Kaskazini, wamejitolea kuwa kwenye mkondo bora wa maisha na hata kuwa kielelezo bora kwa wengine kijijini.

Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Kiambu Bi Ann Wamuratha amefanya jambo la busara ili kuwaleta pamoja vijana hao.

“Lengo langu kuu ni kuona vijana hao wanakuwa raia wema na hata nitataka wajiunge pamoja kufanya miradi tofauti vijijini,” alisema Bi Wamuratha.

Mnamo Ijumaa wiki jana, kiongozi huyo alizuru eneo la Makwa ili kujumuika pamoja na vijana hao na kuelewa changamoto zinazowakabili.

Kulingana na maoni yao, vijana hao walisema tayari wameacha ulevi na matendo maovu katika jamii na badala yake wanataka ufadhili wa kifedha ili waanze kuendesha miradi tofauti.

Mradi wa kwanza muhimu ni kujihusisha na upanzi wa miti ambapo mbunge huyo aliahidiwa kuwanunulia tangi kubwa la kuhifadhi maji ya kunyunyizia miche ya miti.

Katika hafla hiyo mbunge huyo pia alizindua matibabu ya bure siku hiyo kwa wakongwe zaidi ya 500, ambapo walinufaika kwa kupimwa maradhi tofauti na kupata dawa.

Baadhi ya wakongwe hao walipatikana na kisukari, matatizo ya damu, matatizo ya mifupa na maradhi ya macho.

Wakati huo huo pia wanafunzi kadha walio katika shule za upili na vyuo walipokea basari ya Sh7 milioni.

“Singetaka kuona wanafunzi wakibaki nyumbani bila kurejea shuleni kwa sababu ya kukosa karo,” alisema mbunge huyo.

Aliwashauri wazazi wawe macho kwa kuwashauri wana wao wasije wakajihusisha na tabia mbaya na kupotoka.

“Nyinyi wazazi mna majukumu ya kuwalinda watoto wenu. Mzazi ni lazima ujue mienendo ya mtoto kila mara anapokuwa likizoni,” alisema kiongozi huyo.

Alisema ataunga mkono kujengwa kwa kituo cha kutoa ushauri nasaha kwa sababu vijana wengi waliokuwa waraibu wa ulevi wanastahili ushauri kamili.

Alisema atatumikia kila mkazi wa Kiambu bila mapendeleo.

  • Tags

You can share this post!

Wito watoto wanaoishi na ulemavu watunzwe vizuri

Vieira akubali mikoba ya kunoa kikosi cha Strasbourg

T L