• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
MCA sasa ndio wafalme na malkia wapya vijijini

MCA sasa ndio wafalme na malkia wapya vijijini

NA ELVIS ONDIEKI

WAWAKILISHI wa wadi (MCA) wanaowakilisha wapigakura katika Mabunge ya Kaunti wamegeuka kuwa wafalme na malkia wa vijijini kwa umaarufu tofauti na madiwani wa zamani.

Wawakilishi hawa wamekuwa maarufu na kuheshimiwa, huku wakitembea na mabaunsa kila wanakohudhuria hafla tofauti mashinani.

Ndio wanaosikizwa zaidi kuliko walimu na viongozi wengine waliosoma hata kuwashinda.

Makamu Chansela wa Chuo Kikuu cha Maseno Profesa Julius Nyabundi anasikitika kwamba wasomi hawatambuliwi na kuheshimiwa kuliko madiwani wa siku hizi.

“Ninahudhuria mazishi na hafla za kijamii katika vijiji na ni nadra sana kupewa fursa ya kusalimia umati. Lakini MCA au mbunge akifika, anakaribishwa kwa nderemo. Wasiwasi ni; Huenda watoto wasione umuhimu wa kutia bidii masomoni,” anasikitika Prof Nyabundi.

Walimu ambao walikuwa wakiheshimiwa huwekwa pembeni.

Bw Beauttah Omanga mwanahabari wa zamani aliyekuwa mmoja wa MCA wa kwanza chini ya Katiba ya 2010 akiwakilisha wadi ya Bogichora, anasema mabunge ya kaunti yaliletea wapigakura matumaini mapya, kwa kuwa na nguvu na majukumu sawa na ya wabunge.

  • Tags

You can share this post!

Karen Nyamu anavyotumia msanii Samidoh kuvuna umaarufu...

YANAYOJIRI: Serikali yajiandaa kuzindua mradi wa mafuta ya...

T L