• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 3:16 PM
Msizungumze na wanahabari bila idhini, Sakaja aonya maafisa City Hall

Msizungumze na wanahabari bila idhini, Sakaja aonya maafisa City Hall

NA WINNIE ONYANDO

MAWAZIRI wa kaunti ya Nairobi sasa wameamriwa kutafuta idhini kutoka kwa Gavana Johnson Sakaja ili kuhudhuria mahojiano mbalimbali kwenye vyombo vya habari.

Katika barua, gavana Sakaja aliwataka mawaziri wa kaunti na maafisa wengine kuomba kibali kabla ya kufanya mahojiano na wanahabari.

“Hii ni kuwaelekeza maafisa wote na mawaziri wa kaunti walioalikwa kufanya mahojiano na wanahabari kuomba kibali kutoka kwa Gavana kabla ya kuhudhuria mahojiano hayo,” barua kutoka kwa Kaimu Katibu wa Kaunti Patrick Analo ikasema.

Kulingana na barua hiyo, maafisa hao wote wanafaa kueleza ikiwa mahojiano hayo ni ya kibinafsi au la.

Hata hivyo, lengo la barua hiyo halijulikani.

Duru zinasema huenda ilitolewa kwa sababu kuna mawaziri wanaoipaka tope serikali ya gavana huyo au huenda kuna mawaziri ambao hawana tajriba.

Mnamo Oktoba, Mwenyekiti wa Jopokazi la kukabiliana na athari za El-Nino katika Kaunti ya Nairobi, Bramwel Simiyu, alisema kuwa kaunti ilikadiria kutumia angalau Sh1 bilioni katika kupunguza athari za mvua ya hiyo na mojawapo ya vifaa ambavyo vilitarajiwa kununuliwa ni maboti ya injini tena yanayoweza kuruka hewani.

“Lazima pia tujiandae kukabiliana na El-Nino. Inapotokea lazima tuwe na ambulensi, magari ya zimamoto, na maboti ya injini yanayoweza kuruka hewani,” Bw Simiyu akasema.

Kauli yake ilizua mjadala kwenye majukwa ya mitandao mbalimbali ya kijamii huku wachangiaji wakipuuzilia mbali kauli yake.

  • Tags

You can share this post!

Polo abaki singo tena kidosho akihepa kulishwa sukumawiki...

Msanii aliyeonja kifungo bila hatia aendeleza mahamasisho...

T L