• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Mung’aro azindua miradi iliyoanzishwa na Kingi

Mung’aro azindua miradi iliyoanzishwa na Kingi

NA ALEX KALAMA

GAVANA wa Kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro amezindua miradi ya afya iliyoanzishwa na aliyekuwa gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi katika Hospitali Kuu ya Malindi.

Katika hospitali hiyo, Mung’aro alizindua chumba cha kuhifadhi damu, jikoni ya kisasa, chumba maalum cha kuhudumia wafanyakazi wa kaunti na hata wa serikali kuu iwapo wataugua.

Majengo hayo ni sehemu ya miradi ambayo ilianzishwa na mtangulizi wake katika awamu ya pili ya uongozi wake.

Kingi kwa sasa ni spika wa bunge la Seneti.

Miradi mingine iliyozinduliwa na kiongozi huyo ambayo ilianzishwa na mtangulizi wake ni Hospitali Kuu ya Marafa na hospitali ya Mtwapa Medical Complex iliyoko eneobunge la Kilifi Kusini.

Miradi pekee ambayo gavana huyo alizindua ambayo haikuanzishwa na mtangulizi wake katika hospitali ya Malindi ni uzinduzi wa wodi ya wanawake na ya wanaume ambazo alikuta zikiwa katika hali mbaya na akazirekebisha na kuziboresha na kuzifanya kuwa bora zaidi.

Na katika hospitali ya Marafa Mung’aro aliweka vifaa vya kuhudumia wagonjwa kama vile mitambo ya kupiga picha ya Radiology na mingineyo huku katika hospitali ya Mtwapa pia akiweka mitambo sawia na hiyo na kuzifanya hospitali hizo kuwa na uwezo wa kutoa huduma bora za afya za kiwango cha Level 4.

Katika wodi hizo kuna vitanda vipya vya kisasa na ambulensi mpya za kubeba wagonjwa katika hospitali.

Akizungumza baada ya kuzindua miradi hiyo katika hospitali ya Malindi, gavana Mung’aro alisema kwa muda wa mwaka mmoja tangu aingie uongozini, serikali yake imetumia jumla ya Sh344 milioni kuboresha huduma za afya kwenye hospitali mbalimbali za kaunti hiyo.

“Nafikiri mmeona leo tumezindua rasmi miradi ya afya hapa katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wagonjwa wetu sasa watalala katika vitanda vipya. Pia tumerekebisha wodi mbili za wanawake na ile ya wanaume ambazo zilikuwa katika hali mbaya. Wagonjwa pia watakula chakula kizuri sio mambo ya kila siku sima na kabeji,” alisema Bw Mungaro.

Hata hivyo, mchanganuzi wa maswala ya kisiasa katika kaunti hiyo Alfred Katana anahisi kuwa gavana huyo anatumia miradi ya Kingi kujipigia debe kisiasa.

  • Tags

You can share this post!

AMINI USIAMINI: Samaki anayewinda kwa kutema maji kama...

Hatima ya Sheria ya Fedha ya 2023 kuamuliwa Novemba 24

T L