• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Mwanamume anayedaiwa kuwaua kwa kuwachinja wanawe akamatwa

Mwanamume anayedaiwa kuwaua kwa kuwachinja wanawe akamatwa

NA MWANGI MUIRURI 

MWANAMUME anayedaiwa kuwaua kwa kuwachinja wanawe wawili wa kiume wa umri wa miaka mitatu na saba mnamo Jumapili usiku ametiwa mbaroni mjini Maragua mnamo Agosti 8, 2023 akijifanya ni mtu mwenye akili punguani.

Kwa mujibu wa Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Gitonga Murungi, wananchi ndio walimuona mshukiwa huyo kwa jina Evans Kang’ethe,28, akijaribu kuingia mji wa Gakoigo akiwa amebeba gunia na kuvalia kichokoraa huku akichekacheka akitembea.

“Wananchi walimfuata kwa karibu na nikapokezwa ujumbe kwamba kulikuwa na shaka kuu kumhusu. Nilimpigia simu naibu wangu Bw Joshua Okello aliye na afisi mjini Maragua nikimuomba akimbie pahala hapo kutoa mwelekeo,” akasema Bw Murungi.

Bw Okello kufika hapo anasema alimtambua mshukiwa kutokana na picha iliyokuwa imesambazwa na wapelelezi kuhusu mshukiwa wa mauaji ya watoto wake.

“Nikisaidiana na raia, tulimwasilisha hadi katika kituo cha polisi cha Maragua ambapo atasafirishwa hadi kaunti ndogo ya Kiharu kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria,” akasema Bw Okello.

Mauaji hayo ya kinyama yalifanyika katika kijiji cha Mugua Nyoni.

Walioangamia ni Samuel Irungu,7, na Britton Mwangi,3.

Majirani walisema kwamba mshukiwa alikuwa ametengana na mke wake wiki moja iliyopita na siku chache kabla ya mauaji hayo kutokea, alikuwa amemshambulia babake mzazi akimulazimisha kumpa urithi.

“Sisi katika kijiji hiki sasa tuko na uchungu. Tumekerwa sana na kisa hiki. Ashukuru tu Mungu kwamba serikali imempata kabla ya pengine kuteremshuwa adhabu ya umma,” akasema Bi Alice Njogu ambaye ni jirani.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Murang’a Bw Mathiu Kainga alisema amefurahia hatua ya maafisa kufanya juu chini na kushirikiana na raia wema kufanikisha kukamatwa kwa mshukiwa huyo.

  • Tags

You can share this post!

CHARLES WASONGA: Matamshi ya Ruto, Raila yasivuruge...

Utawala wa kijeshi wafunga anga ya Niger

T L